Timu ya Kenya Police Bullets Yabanduliwa katika mashindano ya CECAFA
Timu ya Kenya Police Bullets imebanduliwa katika mashindano ya CECAFA kuwanai kufuzu kwa fainali za kombe la klabu bingwa barani Afrika miongoni mwa akina dada baada ya kulazwa mabao 4-2 na Jeshi La Kujenga Taifa, JKT Queens ya Tanzania, kupitia kwa mikwaju ya penalty wakati wa mchuano wa nusu fainali ulioandaliwa katika uwanja wa Moi Kasarani. Timu hizo mbili zilitoka sare bao moja kwa moja katika muda wa kawaida na wa ziada na mikiki ya penalty ilitumiwa ili kumuamua mshindi.JKT ilifunga mikwaju yake ya penalty kupitia kwa Winfrida Mzoefu, Aaliyah Salu, Melissa Minja na Bahera Crista ilhali Police ilipoteza mikwaju yake miwili iliyopigwa na Emily Moranga na Leah Andiema. Kufuati ushindi huo JKT Queens sasa itamenyana na Rayon Sports ya Rwanda katika fainali ya michuano hiyo. Rayon iliinyuka Kampala Queens mabao 4-3 kupitia kwa mikwaju ya penalty katika mchuano mwingine wa nusu fainali ulioandaliwa jumapili. Fainali ya mashindano hayo imepangwa kuandaliwa tarehe 16 mwezi huu huku mshindi akijinyakulia tikiti ya kuliakilisha eneo la CECAFA katika mashindano kuwania ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika yatakayoandaliwa mwezi Novemba.
Read More