Willy Paul Afungua Rasmi Duka la Pombe “Pozze Liquor” Jijini Nairobi

Willy Paul Afungua Rasmi Duka la Pombe “Pozze Liquor” Jijini Nairobi

Msanii maarufu wa muziki nchini Kenya, Willy Paul, amejiunga rasmi na biashara ya vinywaji baada ya kuzindua duka lake jipya la pombe linaloitwa Pozze Liquor. Duka hili limefunguliwa katika jengo la Safari Business Arcade, barabara ya USIU, jijini Nairobi. Kupitia mitandao ya kijamii, Willy Paul alithibitisha ufunguzi huo rasmi na kuwakaribisha mashabiki pamoja na wateja wote kutembelea duka hilo. Mwanamuziki huyo amesema lengo lake ni kutoa vinywaji vya ubora wa juu huku akichangia katika kukuza ajira kwa vijana. Willy Paul, anayejulikana kwa hits kali kama “Sitolia” na “Tamu Walahi”, anaendelea kupanua wigo wake wa biashara huku akitumia umaarufu wake kuvutia wateja kwenye sekta mbalimbali. Mashabiki wake wameonyesha furaha na kumpongeza kwa hatua hiyo mpya ya kibiashara, wakimtakia mafanikio mema katika safari yake ya ujasiriamali.

Read More
 Willy Paul Kufungua Duka la Pombe, Atangaza Ajira kwa Wataalamu

Willy Paul Kufungua Duka la Pombe, Atangaza Ajira kwa Wataalamu

Msanii maarufu wa Kenya, Willy Paul, ametangaza kuingia rasmi katika biashara ya vileo kwa kuzindua duka lake jipya la pombe linaloitwa PoZZe Liquor. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul alichapisha bango la matangazo ya ajira lenye kichwa kikubwa kisemacho: “PoZZe LIQUOR – Tunatafuta Wafanyakazi.” Tangazo hilo linaeleza kuwa wanahitaji wataalamu pekee walio na uzoefu wa angalau miaka miwili katika biashara ya vileo, na kuwataka waliovutiwa kutuma wasifu wao (CV) kupitia DM ili kupanga usaili. Katika maelezo ya picha hiyo, aliongeza: “Kuna Kitu Kikubwa Kinakuja, @pozze_liquor Inatafuta Wafanyakazi”, akidokeza kuwa huu ni mwanzo wa mradi mkubwa zaidi wa kibiashara. Tangazo hilo limezua msisimko na hamasa miongoni mwa mashabiki wake, wengi wakionekana kuwa na shauku ya kujua zaidi kuhusu kile ambacho msanii huyo anapanga kufanya kupitia chapa yake mpya. PoZZe Liquor inaongeza jina la Willy Paul kwenye orodha ya wasanii wanaopanua shughuli zao hadi kwenye ujasiriamali, hali inayoonyesha jinsi tasnia ya burudani inavyoendelea kuwa jukwaa la mafanikio ya biashara kwa watu maarufu.

Read More