Prezzo awachana mastaa wanaodanganya umri wao kwenye mitando ya kijamii

Prezzo awachana mastaa wanaodanganya umri wao kwenye mitando ya kijamii

Rapa Prezzo amewachana wasanii nchini Kenya wanaodanganya kuhusu miaka yao halisi ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameshangazwa na kasumba hiyo ambayo imekithiri sana miongoni mwa mastaa nchini huku akisema kuwa ni jambo la aibu kwao kuficha umri kwa ajili ya kuwafurahisha walimwengu. Rapa huyo mkongwe amewataka mastaa hao kuacha kadhi ya kupunguza umri na badala yake wamshukuru mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai. “It puzzles me when folks are ashamed of their age. I mean instead of giving thanks for the gift of life they try source for a calculator that can deduct their age or something. Shit is trimilising!” Aliandika.

Read More
 PREZZO AFUNGUKA SABABU ZA KUVALIA VAZI LA KUZUIA RISASI

PREZZO AFUNGUKA SABABU ZA KUVALIA VAZI LA KUZUIA RISASI

Rapa Prezzo amefunguka sababu za kuvalia vazi la kuzuia risasa kwenye mwili anapotoka nyumbani kwake. Katika mahojiano yake hivi karibuni Prezzo amesema alichukua maamuzi ya kuhimarisha usalama baada ya kuvamiwa na majambazi miaka kadhaa iliyopita ambapo wamlipiga risasi kadhaa huku wakitoweka na mali ya thamani ya shillingi millioni 3.5 za Kenya. “When it comes to security; there is no second guessing because I have been shot before at close range. That’s why I know I am here for a reason. So anybody watching this make sure when you come, aim for the head,” Prezzo alieleza Utakumbuka mwaka wa 2020 Prezzo aliweka wazi tukio lilomuacha na makovu ya risasi kichwani kwa kusema kwamba majambazi walimvamia siku chache kabla harusi yake na aliyekuwa mke wake Daisy Kiplagat.

Read More
 PREZZO AFUNGUKA BAADA KUPOTEZA UBUNGE KASARANI

PREZZO AFUNGUKA BAADA KUPOTEZA UBUNGE KASARANI

Rapa wa Kenya Prezzo amefunguka mara ya kwanza baada ya kupoteza kiti cha ubunge eneo la kasarani kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika juzi kati. Katika mahojiano Prezzo amesema ingawa hakubahatika kushinda  kiti cha bunge Kasarani ataendelea kuwafanyia kazi wananchi huku akijitayarisha kuwania tena kiti hicho mwaka wa 2027. Hitmaker huyo wa “Mafans” amesema hajawahi poteza kitu chochote anachokitamani katika maisha yake na hatua ya kushindwa kwenye kinyanganyiro cha ubunge kasarani kwenye uchaguzi mkuu nchini kenya ni anguko lake la kwanza maisha. Hata hivyo anaamini kushindwa kwake kwenye ubunge kasarani ilitokana na yeye kutotoa pesa ikilinganishwa na wapinzani wake ambao walikuwa wanawahonga wananchi ili wawape kura

Read More
 PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

Rapper Prezzo, Sanaipei tande na Mchekeshaji maarufu nchini ambaye pia ni mgombea wa ubunge langat  Jalang’o wametajwa kuwa miongoni mwa mastaa 10 na wachekeshaji 17 wa kenya  ambao watarajiwa kushirikishwa  kwenye show mpya ya ucheshi iitwayo Roast House. Show hiyo inalenga kusherekea mafanikio na machango wa mastaa mbali mbali nchini Kenya kupitia ucheshi ambao utafanywa na kundi la wachekeshaji wa majukwaani. Roast House ina maonyesho au Episodes 10 za dakika 24 kila moja ambayo itawapa nafasi kwa wachekeshaji kutoa burudani na vichekesho wakiangazia madai, kauli mbiu na matukio mbali mbali maishani kwa ajili mastaa watakao kuwa wamealikwa. Roast House ambayo itaruka hewani Julai 14 mwaka huu imetayarishwa na eugene mbugua kwa ushirikiano na D & R studios pamoja na makundi ya wachekeshaji kutoka nchini Kenya.

Read More
 PREZZO AIDHINISHWA NA IEBC KUWANIA UBUNGE

PREZZO AIDHINISHWA NA IEBC KUWANIA UBUNGE

Rapper aliyegeukia siasa Jackson Ngechu maarufu Prezzo ameshindwa kuficha furaha yake baada ya tume ya IEBC kumuidhinisha kuwa atawania ubunge wa eneo la Kasarani kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kupitia Tiketi ya chama cha Mabadiliko Na Busara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Prezzo amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba amekithi vigezo vyote ambavyo tume ya IEBC ilikuwa inahitaji kutoka wagombea huru ya kuwasilisha saini 1,000 huku akidokeza mpango kuanza kuomba uungwaji mkono kutoka kwa wananchi. “The Revolution Shall Be Televised! IEBC Requirements For An Independent Ticket Was 1000 Signatures. Iam Happy To Say That We Surpassed That & Now It’s Time To Hit The Grounds. Chama Madiliko Na Busara! #CMB #PrezzoForKasarani #NgwareNaMapema“, ameandika Instagram. Prezzo anaungana na Wasanii wengine walioidhinishwa na IEBC kama Bahati anayewania ubunge Mathare kupitia Tiketi ya Jubilee, mchekeshaji Jalang’o ambaye ni mgombea wa ubunge Lang’at kupitia cha cha ODM, Gabu anayewania Mwakilishi Wadi ya Woodley Golf Course kupitia Chama cha AMANI na MC Jessy ambaye ni mgombea wa ubunge, Imenti Kusini.

Read More