Geosteady akanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash

Geosteady akanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash

Msanii kutoka nchini Uganda Geosteady amekanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash kufuatia uvumi unaosamba mtandaoni kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi. Kwenye mahojiano na karibuni yake amesema ukaribu wao ulikuwa ni kwa ajili ya kuitangaza show yake itakayofanyika leo aliyoipa jina “Dine With Geosteady” “Alionekana tu kwa video yangu. Hakuna kitu kingine zaidi ya hiyo. Tuna ukaribu kwa sasababu ananisaidia kutangaza show yangu. Sisi sio wapenzi”, Alisema. Geosteady na Prima Kardashi ambao wana watoto watatu kwa pamoja walivunja mahusiano yao miaka mitatu iliyopita na kila mmoja akaingia kwenye mahusiano mengine. Prima alikuwa kwenye mahusiano na Mr.Henrie lakini wakavunja mahusiano yao huku Geosteady akianzisha mahusiano na mrembo aitwayo Hindu kisha baadae akahamia kwa Minaj ambaye wamezaa mtoto mmoja.

Read More
 Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Geosteady ameamua kutoa ya moyoni kuhusu hatma ya uhusiano wake na mzazi mwenzie Prima Kardash. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema hana mpango wa kufunga ndoa hivi karibuni na Baby Mama wake huyo. Kulingana na Hitmaker huyo wa “Sembera”, alipoteza hamu ya kuwa kwenye ndoa na Kardash kutokana kujihusisha na vitendo vya usaliti. “Sioni nikimuoa Prima, nilikuwa na maono hayo hapo nyuma lakini sina tena,” Geosteady alifichua. Geosteady na Prima ambao walifufua penzi lao miezi kadhaa iliyopita kwa pamoja wana watoto wawili.

Read More