Miss Omuts Amshutumu Pritty Vishy kwa Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu BBL

Miss Omuts Amshutumu Pritty Vishy kwa Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu BBL

Mjadala mkali umeibuka mtandaoni baada ya Digital Creator, Miss Omuts, kumtuhumu mrembo aliyegeukia maisha ya Usosholaiti Pritty Vishy kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu kufanya upasuaji wa kuongeza makalio maarufu Brazilian Butt Lift (BBL). Kupitia mitandao ya kijamii, Miss Omuts amedai kuwa madai ya Vishy hayana ukweli wowote, akieleza kwamba mtu anayefanyiwa BBL hawezi kukaa chini mara moja kutokana na maumivu makali yanayoambatana na upasuaji huo. Kauli hii imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wafuasi wa pande zote mbili, huku baadhi wakimtetea Pritty Vishy na wengine wakiunga mkono hoja za Miss Omuts. Hayo yote yameibuka baada ya Pritty Vishy kuibua gumzo mtandaoni kuhusu maisha yake binafsi, hasa baada ya kudai kuwa alitumia zaidi ya shillingi milioni moja kubadilisha muonekano wa mwili wake kwa upasuaji wa kuongeza makalio kwa mafuta (BBL), kuondoa mafuta ya ziada mwilini (liposuction), na kuondoa ngozi na mafuta tumboni (tummy tuck).

Read More
 Pritty Vishy Afichua Gharama Halisi za Upasuaji Wake wa Urembo

Pritty Vishy Afichua Gharama Halisi za Upasuaji Wake wa Urembo

Mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii nchini Kenya, Pritty Vishy, ameweka wazi gharama kamili alizotumia kubadilisha mwonekano wa mwili wake kupitia upasuaji wa urembo. Akizungumza kuhusu safari hiyo, Vishy alisema alitumia kati ya KSh 1.2 milioni na KSh 1.5 milioni, kinyume na uvumi ulioenea mitandaoni uliodai alitumia KSh 500,000 pekee. Upasuaji huo ulihusisha kuboresha makalio kwa mafuta (Brazilian Butt Lift – BBL), kuondoa mafuta ya ziada mwilini (Liposuction), na kuondoa ngozi pamoja na mafuta tumboni (Tummy Tuck). Alifafanua kuwa sehemu kubwa ya bajeti hiyo ilihusisha Tummy Tuck iliyogharimu kati ya KSh 350,000 na 400,000, Lipo 360 iliyogharimu kati ya KSh 300,000 na 350,000, pamoja na BBL iliyomgharimu KSh 500,000. Gharama hizo pia zilijumuisha huduma za baada ya upasuaji kama vile massages, vifaa muhimu na ukaguzi wa kitabibu. Vishy aliongeza kuwa alitumia kati ya KSh 400,000 na 500,000 kwa dawa ya Ozempic, inayotumika kudhibiti uzito, jambo lililoongeza zaidi gharama za safari yake ya kubadilisha muonekano. Kauli yake imeibua mjadala mitandaoni, huku wafuasi wake wakitofautiana kuhusu maamuzi yake na kiwango kikubwa cha fedha alichowekeza katika mwonekano wake wa sasa.

Read More
 Khaligraph Jones Afichua Kupunguza Kilo 22 Kwa Miezi Mitatu Kupitia Mazoezi na Kula kwa Mpangilio

Khaligraph Jones Afichua Kupunguza Kilo 22 Kwa Miezi Mitatu Kupitia Mazoezi na Kula kwa Mpangilio

Rapa maarufu wa Kenya, Khaligraph Jones, amefichua safari yake ya kupunguza uzito, akisema kuwa ameweza kupunguza kilo 22 ndani ya miezi mitatu pekee. Akiweka wazi safari yake ya afya kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Khaligraph  alieleza kuwa awali alikuwa na uzito wa 137 kg, lakini sasa ana uzito wa 115 kg, hatua aliyofikia kwa kutumia mbinu ya intermittent fasting (kula kwa mpangilio wa muda) pamoja na mazoezi ya mwili. “Nilikua nakula ngwashe, maji na apple,” alisema rapa huyo, akionyesha kuwa mlo wake ulikuwa mwepesi lakini wenye afya. Katika mahojiano, Khaligraph pia alimpongeza mwanamitandao maarufu nchini Pritty Vishy kwa jitihada zake za kupunguza uzito, akisema kuwa alihamasishwa na kujitolea kwake, hasa alipokuwa akifanya mazoezi pamoja na mkewe. “Vishy alikua anajitahidi sana. Ilikua motisha pia kwangu,” alisema. Aidha, Khaligraph amepuuzilia mbali madai yanayosambaa mtandaoni kuwa Pritty Vishy hutumia dawa kupunguza mwili wake. Alisisitiza kuwa madai hayo hayana msingi na kwamba mafanikio ya Vishy yanatokana na bidii na nidhamu ya hali ya juu. Mashabiki wengi wamepongeza uamuzi wa Khaligraph wa kuchukua hatua za kuboresha afya yake na kuonyesha mfano kwa wengine kuwa inawezekana kupunguza uzito kwa njia salama na za asili.

Read More
 Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Mtengeneza maudhui nchini Kenya Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wamewaacha mashabiki wakijiuliza maswali iwapo wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi. Hii ni baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonesha Pritty Vishy akimnyanyua Becky walipokuwa wakicheza muziki na kisha wakaendelea kupigana mabusu. Lakini pia walichapisha video nyingine kwenye TikTok live wakiwa kwenye mahaba mazito kwenye mazingira ya klabu. Mashabiki wao kwenye mtandao wa TikTok walitoa hisia tofauti huku wengi wakihoji kuwa huenda wawili hao wanaodai kuwa marafiki wa karibu wameanza kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita Pritty Vishy alionyesha nia ya kimapenzi kwa mwimbaji wa nyimbo za injili Daddy Owen baada ya mwimbaji huyo kufichua kwamba alikuwa anatafuta mke wa kuingia nae kwenye ndoa. Mwanamuziki huyo hata hivyo alikataa ombi lake akidai kuwa foleni ya wanawake wanaotaka kimapenzi ilikuwa ndefu

Read More
 Pritty Vishy akata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen.

Pritty Vishy akata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen.

Mrembo asiyeishiwa na matukio kila leo Pritty Vishy amekata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen ikiwa ni siku chache zimepita toka mwimbaji huyo wa injili amkatae hadharani. Mrembo huyo ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuwa penzini na msanii Stivo Simple Boy amemtaja Daddy Owen kama dikteta asiyekuwa na msimamo mara baada ya kusisitiza kuwa mwanamke wa ndoto yake lazima ajue kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha lakini pia asiwe mtumiaji wa mtandao wa Tiktok. Hata hivyo amemalizia kwa kumshauri hitmaker huyo wa Vanity kutimukia nchini Uganda iwapo anataka kufanikisha mchakato wa kupata mke wa kuingia naye kwenye ndoa kwani wasichana wa Kenya hawana ufasaha wa lugha ya Kiingereza. “Nilikua namtaka lakini sasa penye inaelekea ni kama itabidi avuke Uganda. He’s like a dictator. Sijui hataki dem ako TikTok, anataka dem anajua Kizungu mingi. Ikifika mahali ya TikTok na Kizungu mingi avuke tu Uganda. Hapa Kenya tuko TikTok na tunaongea Kizungu ya kilami. Ugandans ndio wako bushy,” Alisema. Utakumbuka mara baada ya Daddy Owen kutangaza kuwa anatafuta mke wa kuingia naye kwenye ndoa mapema wiki iliyopita, amepokea zaidi ya maombi 10,000 kutoka kwa wanadada tofauti ambao wametia nia ya kumtaka kimahusiano.

Read More
 Penzi la Pritty Vishy na Madini Classic laingiwa na ukungu

Penzi la Pritty Vishy na Madini Classic laingiwa na ukungu

Mrembo maarufu mtandaoni nchini Pritty Vishy amethibitisha kutokuwa na maelewano mazuri na mchumba wake msanii Madini Classic. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mrembo huyo amesema kwa muda sasa hawajakuwa pamoja na Madini Classic kutokana na ugomvi ulioibuka kati yao juzi kati. Vishy amedai kwamba kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutatua tofauti zao huku ukisisitiza kuwa ikitokea hawatapa mwarubaini wa ugomvi wao huenda wakavunja mahusiano yao rasmi. Kauli ya Pritty Vishy imepingwa vikali na Madini Classic ambaye amedai kuwa hawana tofauti zozote na mrembo huyo huku akikazia kuwa penzi lao lipo imara licha ya kutoonekana wakiwa pamoja katika siku za hivi karibuni.

Read More
 Pritty Vishy azua gumzo mtandaoni, Akiri kuwahi kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Pritty Vishy azua gumzo mtandaoni, Akiri kuwahi kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Mchumba wa msanii Madini Classic, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kukiri hadharani kuwahi kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Kupitia insta stori yake kwenye mtandao wa Instagram mrembo huyo amesema alikuwa anavutiwa kimapenzi na wanawake wenye makalio makubwa. ” Mi nishawahi, Ilikua dame tulikutana naye Facebook. Nlikuwa curious kujua lesbians hufanya nini. Si tukaslide mpaka Whatsapp. Akanituamia nudes zake na akaniambia nimgtumie zangu. na Nikatuma mpaka video.” alisema akijibu shabiki yake aliyetaka kufahamu kama amewahi kuvutiwa na wanawake wenzake kimapenzi. Pritty vishy alipata umaarufu nchini baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Stivo Simple Boy lakini walikuja wakaacha kwa madai ya usaliti. Kwa sasa mrembo huyo yupo kwenye mahusiano mengine na msanii Madini Classic mahusiano ambayo yameanza kuyumba kutokana na wawili hao kutokuwa na ukaribu tofauti na walivyokuwa wanatambulisha mahusiano yao kwa umma.

Read More
 PRITTY VISHY AFUNGUKA SABABU ZA KUTOHUDHURIA HARUSI YA STIVO SIMPLE BOY

PRITTY VISHY AFUNGUKA SABABU ZA KUTOHUDHURIA HARUSI YA STIVO SIMPLE BOY

Ex wa msanii Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni baada ya kukiri hadharani kuwa atahudhuria harusi ya mkali huyo wa ngoma ya Freshi Barida. Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram vishy amesema anaogopa makalio yake yaatamchanganya kimawazo Stivo kwenye siku yake hiyo muhimu. Sanjari na hilo amesema haoni ndoa ya Stivo na mpenzi wake Gee ikidumu kwa kuwa anajua uyonge wa msanii huyo linapokuja suala la unyumba. Hata hivyo amemtolea uvivu msanii huyo wa Men in Business kutokana na suti aliyokuwa amevaa juzi kati kwa kusema kwamba mtindo wa suti hiyo ni wa kizamani sana, hivyo waliomvalisha walifeli kinoma. Utakumbuka Vishy ambaye anaidaiwa kutoka kimapenzi na msanii Madini Classic alikuwa kwenye mahusiano na Stivo Simple Boy lakini walikuja wakaachana kutokana na madai ya usaliti.

Read More
 MADINI CLASSIC AWAJIBU WANAMKOSOA MPENZI WAKE PRITTY VISHY

MADINI CLASSIC AWAJIBU WANAMKOSOA MPENZI WAKE PRITTY VISHY

Msanii kutoka Mombasa Madini Classic amelazimika kumkingia kifua mpenzi wake mpya baada ya rafiki yake kudai kwamba ikiwa atamuoa Pritty, hatamzalia watoto wazuri. Kupitia ukurasa wake wa instagram, Madini amesema kuwa mchumba wake Pritty si kama wanawake wengi kwa sababu huwa Hariri picha anazoziweka kwenye mitandao yake ya kijamii. “Sielewi ni kwa nini wengi wenu mnafikiri Pritty si mrembo ni kwa sababu hachapishi picha zilizohaririwa mtandaoni kama baadhi yenu? Get to meet that chil physically utakubaliana nami that’s cute,” Madini aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Habari za wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusambaa mapema mwezi uliopita, ambapo walikuja wakathibitisha kuwa ni wapenzi na hata wakaanza kusambaza picha zao wakiwa kwenye pozi za kimahaba zaidi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na blogu mbali mbali.

Read More
 PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

Msanii Madini Classic amethibitisha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Ex wa Stivo Simple Boy Prity Vishy ikiwa ni miezi kadhaa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja. Katika mahojiano yake hivi karibuni Madini amesema alianza mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii alipomtumia ujumbe mfupi mrembo huyo na kumuomba namba ya simu huku akisema kwamba ujasiri na uhalisi wake ndio ilivutia sana. “I met her on Instagram, I texted her and asked for her mobile number. We started there. I like her courage and she’s real,” Amesema Madini. Hitmaker huyo wa ngoma ya Nilivyo amesema alipoweka wazi nia yake ya kutaka kumchumbia mrembo huyo, Vishy hakuamini na alisita kwa kuwa kipindi cha nyuma wasanii wengi wamekuwa wakimtafuta kwa ajili ya kufanya nae kazi. Madini Classic amewataka walimwengu kutomshambulia Vishy kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa inamuumiza kwa sana. “It really hurts me when I see people trolling her. She is an amazing personality when you get to interact with her and the trolls bring her energy down,” Amesema. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutilia shaka madai ya Madini Classic na Pritty Vishy wakidai kuwa wana kazi ya pamoja wanafanya hivyo wanatumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni. “Ati babe…ata haiendani. Hii clout haijaenda shule bado.”  Shabiki mmoja ameandika kwenye Instagram.  

Read More
 PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

Mpenzi wa mwanamuziki Stivo The Simple, Pritty Vishy ameonekana kukerwa na kitendo cha msanii Adasa kuonekana kumzimia kimahaba rapa huyo kwenye moja ya video aliyoshare kwenye mtandao wa Instagram. Kwenye video hiyo ambayo wapo ufukweni mwa bahari Hindi, Adasa anaonekana akipiga stori na Stivo the Simple wakiwa matembezini ambapo ghafla aliaanza kumzungushia kiuno akiwa katika pozi la kimahaba zaidi, jambo ambalo lilimfanya Pritty Vishy ashuke kwenye uwanja wa comment ya post hiyo na kumpa Adasa somo akae mbali na mpenzi wake Stivo The Simple Boy, la sivyo atamfunza adabu. Hata hivyo Adasa alishindwa kumvumilia vitisho vilivyotolewa na mrembo huyo ambapo nae aliamua kujibu mapigo kwa kujitapa kwamba wakati Pritty Vishy kuwa na Stivo The Simple Boy kimahusiano ulishaisha kitambo, hivyo ni zamu yake kumuonesha msanii huyo mapenzi mujarab. Sasa baada ya kutunishiana misuli kwenye mtandao wa Instagram Prityy Vishy aliamua kwenda live instagram akiwa mwenye huzuni huku akiilaani vikali   kitendo cha Stivo the simple boy kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na Adasa ambaye kwa mujibu amzidi na chochote. Hata hivyo hatua ya wawili hao kurushiana maneno makali hadharani kisa mwanaume imeibua hisia miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambao wamehoji kuwa huenda wawili hao wanajaribu kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kabla ya ujio wa ngoma mpya ya Stivo The Simple aliyomshirikisha Adasa.

Read More
 PRITTY VISHY ATANGAZA KUVUNJA UHUSIANO WAKE WA KIMAPENZI NA MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

PRITTY VISHY ATANGAZA KUVUNJA UHUSIANO WAKE WA KIMAPENZI NA MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

Mchumba wa msanii Stivo The Simple Boy ametangaza kuachana na msanii huyo baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda. Akipiga stori na mzuka kibao Pritty Vishy amesema amechukua maamuzi ya kuachana na Stivo the simple baada ya msanii huyo kuonekana kutomdhamini kwani amekuwa akiusikiliza sana uongozi wake wa Made In Kibera. Kauli ya Pritty Vishy inakuja siku chache baada kudai kuwa uongozi wa Made in Kibera umekuwa ukimnyanyasa Stivo the Simple kwa kupora pesa zake ambazo amezitolea jasho kupitia muziki. Hata hivyo Stivo The Simple hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya Pritty Vishy ila ni jambo la kusubiriwa

Read More