PROFESSOR JAY ADOKEZA KOLABO YAKE NA G-NAKO

PROFESSOR JAY ADOKEZA KOLABO YAKE NA G-NAKO

Nyota wa muziki wa Bongofleva Professor Jay ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha G-nako. Rapa huyo mkongwe wa muziki nchini Tanzania ametuweka wazi hilo kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii huku picha ikimuonesha akiwa studio na mtayarishaji Bin Laden wa Tongwe Records. Ni muendelezo wa Kolabo zake na vijana wa sasa kwenye muziki wa bongo fleva, ngoma ambayo ipo masikioni mwetu kwa sasa ‘Shikilia’ amewapa mashavu wakali wa kizazi hiki kama Maua Sama na Young Lunya. Ni miezi Nane sasa tangu Prof Jay kuanza kushusha mangoma makali, mkwaju wake wa kwanza ulikuwa ‘Utaniambia nini’

Read More
 PROFESSOR JAY ATANGAZA UJIO WA EP MPYA

PROFESSOR JAY ATANGAZA UJIO WA EP MPYA

Staa mkongwe wa muziki wa rap nchini Tanzania, Professor Jay ameweka wazi kuachia EP mpya yenye jumla ya ngoma 5 hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa instagram Professa Jay ameandika ujumbe unaosomeka “Badala ya kuwapa chakula cha ubongo kwa single moja naona kama niwape chakula cha EP ya nyimbo 5 au mnasemaje Maboss wangu” Professa Jay amebainisha hilo ikiwa ni takribani miezi 6 imepita tangu alipoachia hitsong yake iitwayo “Utanambia Nini”.

Read More