PUSHA T AFUNGUKA SABABU ZA KUMALIZA UGOMVI WAKE NA DRAKE

PUSHA T AFUNGUKA SABABU ZA KUMALIZA UGOMVI WAKE NA DRAKE

Rapa kutoka Marekani Pusha T hatimaye amefunguka sababu iliyomfanya kumaliza bifu yake na Drake ambayo ilidumu kwa miaka 10. Kwenye mahojiano na Desus & Mero, Pusha T ameeleza kwamba, kuwa Baba mwaka 2020 ndio sababu pekee iliyomfanya aimalize bifu yake na Drizzy kwani kulimbadilisha mtazamo wake kwa ujumla hasa kuwahusisha watoto kwenye ugomvi. Kama utakumbuka vyema, Pusha T ndiye aliifahamisha dunia kwamba Drake ana mtoto anaitwa Adonis lakini alimficha. Kupitia freestyle yake ‘The Story of Adidon’ Pusha alichana “You are hiding a child, let that boy come home/ Deadbeat mothaf*cka, playin’ border patrol/ Adonis is your son.” Hii ilimfanya Drake na baadaye kuthibitisha taarifa hizo kupitia album yake, Scorpion mwaka 2018.

Read More