R. Kelly na mchumba wake wapata mtoto

R. Kelly na mchumba wake wapata mtoto

Mwimbaji nguli wa RnB, R.Kelly na mchumba wake, bibie Joycelyn Savage wamepata mtoto wao wa kwanza wakike, aliyepewa jina “Ava Lee Kelly”, ambapo wamepata mtoto huyo kwa njia ya upandikizaji. R.Kelly ambaye kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo chake, mchumba wake huyo amebainisha kujifungua kupitia mfululizo wa post zake katika ukurasa wake wa Instagram pamoja na ku-share picha za kichanga hicho, akieleza kajifungua tarehe 8 mwezi huu. Hata hivyo, sio R.Kelly wala Wakili wake aliyethibitisha ukweli wa taarifa hiyo ikizingatiwa mrembo Joycelyn Savage (pichani) alikuwa ni miongoni mwa wahanga wa vitendo vya kinyama vya msanii R.Kelly ambapo Julai mwaka huu alijitokeza hadharani na kumtetea mwanamuziki huyo huku akisema kwamba walikuwa wachumba na ana ujauzito wake.

Read More
 R. Kelly akanusha kuhusu kuachia Album mpya

R. Kelly akanusha kuhusu kuachia Album mpya

Mkongwe wa muziki wa RnB kutoka nchini Marekani Robert Sylvester Kelly alimaarufu kama R Kelly ameachia album yake licha ya kuwa gerezani. Licha ya kuachia Album hiyo ya aliyoipa jina la I ADMIT IT ikiwa na ngoma 13, Kampuni ya Sony Music iliishusha Album hiyo kwenye majukwaa ya Spotify na Apple Music. Mwanasheria wa Mwanamuziki huyo mkongwe, Jennifer Bonjean amekaririwa na mtandao wa The Hollywood Reporter akisema, Album hiyo ilichiwa bila kuidhinishwa, ni kazi ambayo iliwahi kuibiwa. Bonjean aliendelea kusema kwamba waliwahi kutoa taarifa polisi kwamba kuna baadhi ya ‘Masters’ za R. Kelly ziliwahi kuibiwa lakini hawakufanya uchunguzi wowote. “Pindi anakamatwa, kulikuwa na vifaa vya studio ambavyo vilichukuliwa. Masters zake zilipotea. Kwa hiyo ni nani aliyekuwa nazo na nani anafaidika nazo, hatumfahamu.” Alisema Tunafahamu kwa R Kelly yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka 30 kwa makosa mbalimbali ya unyanaysaji Kingono kwa watoto wenye umri mdogo.

Read More
 R KELLY AKUTWA NA MAKOSA YA KUJIHUSISHA NA PICHA ZA NGONO ZA WATOTO WADOGO

R KELLY AKUTWA NA MAKOSA YA KUJIHUSISHA NA PICHA ZA NGONO ZA WATOTO WADOGO

Mwimbaji mkongwe wa Muziki wa R&B Robert Sylvester Kelly (R Kelly) amekutwa tena na hatia ya makosa 6 kati ya 13 katika kesi zinamkabili ikiwemo kujihusisha na picha za ngono za watoto wadogo. Mwimbaji huyo alishtakiwa katika mji aliozaliwa wa Chicago kwa mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na kutengeneza picha za unyanyasaji wa watoto, kuwashawishi watoto kufanya ngono, yaliyofanyika 2008. Kelly amekutwa na hatia ya makosa hayo katika mahakama ya mjini Chicago Jumanne ya wiki hii. Inaelezwa endapo kukiwa na hukumu juu ya mashtaka hayo sita, adhabu yake huenda ikaanza na miaka 10 hadi 90 jela. Ikumbukwe kwamba kwa sasa R Kelly anatumikia kifungo cha miaka 30 baada ya hukumu yake Juni 29, kwa makosa ya kingono na ulaghai.

Read More
 R. KELLY KUPANDISHWA KIZIMBANI TENA

R. KELLY KUPANDISHWA KIZIMBANI TENA

Mwanamuziki kutoka Marekani R. Kelly kuanza kupandishwa tena kizimbani, shtaka lake la mwaka 2008 ambalo anakabiliwa nalo kwa kujihusisha na masuala ya kutengeneza maudhui ya ngono kwa watoto (Child Pornography) limeanza kusikilizwa Jumatano. Taarifa kubwa ni kwamba Wazee wa Baraza la Mahakama wameruhusiwa kutazama mikanda mitatu ya ngono ambayo Mwanamuziki R. Kelly alikuwa akijirekodi na mabinti hao wadogo kama ushahidi mbele ya Mahakama. Mbali na msumari huo, binti mmoja ambaye jina lake limefichwa, naye ameapa kutoa ushahidi kuwa alifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono huku akirekodiwa na R. Kelly alipokuwa na umri wa miaka 14. Video yake pia itaoneshwa mbele ya wazee wa baraza la Mahakama ili kumtambua R. Kelly ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 Jela

Read More
 R. KELLY APUZILIA MBALI UJA UZITO WA MREMBO JOYCELYN SAVAGE

R. KELLY APUZILIA MBALI UJA UZITO WA MREMBO JOYCELYN SAVAGE

Mwimbaji Robert Kelly maarufu R.Kelly ambaye kwa sasa anatumikia miaka 30 ya kifungo chake gerezani, amekanusha taarifa ya mrembo Joycelyn Savage ambaye ni mhanga katika makosa yake, kudai ana ujauzito wake. Mwanasheria wa Kelly, Jennifer Bonjean ameiambia TMZ hamna ukweli wowote juu ya hilo. Mrembo Joycelyn Savage kupitia chapisho ndani ya kitabu chake kipya kilichotoka Ijumaa ya wiki iliyopita, alitoa taarifa ya kuwa na ujauzito wa Kelly licha ya kutoeleza ni namna gani alipata ujauzito huo, hali ya kuwa R.Kelly amekuwa kwenye mikono ya sheria tangu Julai, mwaka 2019. Aidha, kwenye chapisho la mrembo Joycelyn Savage alieleza kwamba R.Kelly alifurahishwa na taarifa hizo za ujauzito wake

Read More
 R KELLY ATUPWA JELA MIAKA 30

R KELLY ATUPWA JELA MIAKA 30

Mwanamuziki wa Marekani wa miondoko ya R&B, R Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na mabinti wadogo. R. Kelly, amepatikana na hatia ya kulazimisha, kushawishi na usafirishaji wa kingono wa binti aliyekuwa chini ya miaka 18. Tuhuma za uhalifu wa kingono zinazomkabili R. Kelly zilijulikana kwa umma baada ya vuguvugu la Me Too kuanza mnamo mwaka wa 2017. Utakumbuka R. Kelly alikamatwa Februari mwaka wa 2019 kwa madai ya unyanyasaji wa kingono uliokithiri

Read More
 WAENDESHA MASHTAKA WAMTAKA JAJI AMFUNGE R. KELLY MIAKA 25 GEREZANI

WAENDESHA MASHTAKA WAMTAKA JAJI AMFUNGE R. KELLY MIAKA 25 GEREZANI

Waendesha Mashtaka kwenye Kesi ya R. Kelly wamemtaka Jaji amhukumu mwimbaji huyo kutoka Marekani kifungo cha zaidi ya miaka 25 Gerezani. Hii ni baada ya mwezi Septemba kukutwa na hatia ya makosa 9 yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono kwa Wanawake na mabinti wenye umri mdogo. Juni 8 mjini New York, Jopo la Waendesha Mashtaka wa Serikali lilimwambia Jaji kwamba R. Kelly amekimbia hukumu kwa takribani miaka 30, na sasa lazima aende Jela. R. Kelly amepanga kukata rufaa juu ya maamuzi hayo, na inatakiwa afanye haraka kabla ya Juni 29 mwaka huu kwani ndio siku ya kutolewa hukumu.

Read More
 MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

Mauzo ya muziki wa R. Kelly yameripotiwa kupanda kwa asilimia 517 tangu akutwe na hatia ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na mengine. Kwa mujibu wa Rolling Stone, mauzo ya muziki wake kwenye majukwaa ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni (Digital Platforms) yamepanda kutoka millioni 11.2 hadi millioni 13.3 ikiwa ni wiki moja tangu akutwe na hatia ambayo huwenda ikampeleka gerezani miaka 10 au hata kifungo cha maisha. Mitandao kama Apple Music na Spotify ilizima muziki wa R. Kelly, huku wasanii kama Chance the Rapper, Lady Gaga, Ciara na Celine Dion walimfuta kwenye Kolabo za nyimbo ambazo walifanya naye. Mwishoni mwa Wiki iliyopita YouTube ilizifungia akaunti zake mbili za muziki kwenye mtandao huo.

Read More
 CHANNEL ZA R. KELLY YOUTUBE ZAFUNGIWA KUFUATIA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO.

CHANNEL ZA R. KELLY YOUTUBE ZAFUNGIWA KUFUATIA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO.

Kufuatia mashtaka ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo na makosa mengine yanayomkabili nguli wa muziki wa R&B duniani, R. Kelly, mtandao wa Youtube umechukua hatua ya kuzifungia channel rasmi za staa huyo.   Channel hizo ni pamoja na R Kelly TV na R Kelly Vevo ila, nyimbo za nguli huyo bado zipo Youtube kupitia channel za watu wengine.   Kwa sasa R.Kelly anasubiria hukumu yake ambayo imetajwa kutolewa Mei 4 mwakani, na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kifungo cha maisha gerezani.            

Read More