Mwanamuziki Rabadaba afufua penzi lake na baby mama wake Sheila Ferguson
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Rabadaba ameripotiwa kufufua penzi lake na baby mama wake Sheila Ferguson ambaye kwa pamoja wamejaliwa kuwapata watoto wawili. Chanzo cha karibu kimesema Rabadaba alianza kuwa kwenye mahusiano na Ferguson pindi tu alipotua nchini Uingereza na mke wake Maggie. Licha ya kuwa Maggie alitishia kumrejesha Rabadaba nchini kwao uganda kwa kumsaliti kimapenzi, mwanamuziki huyo kwa sasa inaonekana hana wasiwasi kwa sababu mama ya watoto wake Ferguson atamuokoa ikizingatiwa kuwa ana uraia wa uingereza. Ikumbukwe Rabadaba kwa wiki kadhaa sasa amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa madai ya kumsaliti kimapenzi mke wake Nnalongo Maggie baada ya kudumu kwenye ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. Rabadaba ambaye alihamia nchini Uingereza kukaa na Maggie baada ya kuhalalisha ndoa yao, juzi kati mrembo huyo alijitokeza na kudai kuwa msanii huyo alimtumia vibaya kwa ajili ya kupata visa ya kwenda uingereza na baadae akamkimbia.
Read More