Grandpa Records kurejelea tena shughuli zake za muziki mwaka 2023
Muasisi wa Grandpa Records Noah Yusuf maarufu kama Refigah amedokeza mpango wa kuzindua rasmi lebo hiyo ambayo ilikuwa imesitisha huduma zake kutokana na changamoto za kifedha. Kwenye mahojiano na SPM Buzz amesema ameiteua timu mpya ambayo itasimamia shughuli za lebo hiyo mwakani, hivyo hatajihusisha na kazi za lebo hiyo kwa kuwa ataelekeza nguvu zake kwenye kilimo biashara. Rafigah alistaafu muziki mwaka 2007 na akaamua kuwekeza kwenye masuala ya kutayarishaji wa muziki na kuwasimamia wasanii. Mwaka 2009 alizundua rasmi Grandpa Records, lebo ambayo imewatambulisha baadhi ya wasanii tajika nchini baada kusitisha huduma zake mwaka 2017.
Read More