Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Ragga Dee amemkataa Bosi wa Big Talent, Eddy Kenzo. Hii  ni  baada ya watu kuhoji kuwa Eddy Kenzo ndiye mwanamuziki bora nchini humo kufuatia kuteuliwa kwake kwenye tuzo za Grammy mwaka 2023. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ragga Dee amesema kuna wasanii wengi nchini Uganda ambao wana vipaji kumzidi Kenzo, hivyo kwa upande wake haamini kama hitmaker huyo “Nsimbudde” hapaswi kupewa taji la mwanamuziki bora nchini humo. “Eddy Kenzo ni msanii mzuri sana, hata hivyo, sio mwanamuziki bora nchini Uganda. Kuna wasanii wengine wazuri wa Karamoja na mikoa mbalimbali ambao hatuwajui,” alisema. Ikumbukwe kipindi cha nyuma Kenzo alisema kwamba hajali maneno ya watu wanaodai kuwa yeye ni msanii bora nchini uganda, ila jambo analozingatia kwenye muziki wake ni kufanya kazi zenye ubora. Wasanii kadhaa ikiwemo Gravity Omutujju na Roden Y Kabako wanamtaja Eddy Kenzo kama mwanamuziki bora nchini Uganda.

Read More
 Ragga Dee afunguka kustaafu muziki

Ragga Dee afunguka kustaafu muziki

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Ragga Dee amedai kuwa hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni licha ya kuwa hajakuwa akiachia nyimbo katika miaka ya hivi karibuni. Kwenye mahojiano yake na kituo kimoja cha redio nchini uganda Ragga Dee amethibitisha kuwa ataendelea kufanya muziki hadi atakapopumua hewa yake ya mwisho duniani. “Muziki ipo ndani mwangu. Nimekuwa nikifanya tangu utotoni. Siwezi kuacha muziki kamwe. Ragga Dee alieleza. Ragga dee ni moja kati ya wasanii walioacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini uganda na alipata umaarufu zaidi Afrika Mashariki kupitia wimbo wake uitwao “Ndigida.” Mwaka wa 2016 aligeukia siasa kwa kuwania kiti cha umeya wa jiji la kampala kwenye uchaguzi mkuu lakini kwa bahati mbaya alishindwa na Erias Lukwago.

Read More
 RAGGA DEE AKANUSHA TUHUMA ZA KUPORA FEDHA ZA MADEEJAY UGANDA

RAGGA DEE AKANUSHA TUHUMA ZA KUPORA FEDHA ZA MADEEJAY UGANDA

Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Ragga Dee amejitenga na madai ya kufuja pesa za madeejay alizopewa na Gen. Salim Saleh. Hitmaker huyo wa “Letter O” amekanusha tuhuma hizo ambazo ziliibuliwa dhidi yake na Madeejay nchini Uganda wakisema kwamba alikimbia na pesa zao ambazo walipewa na serikali kutokana na makali ya corona. Akiwa kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda Ragga Dee amesema aliupokeza muungano wa madeejay nchini humo shillingi milloni 10 na ilipokelewa DJ Nimrod. Mwanamuziki huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa tamaa imewaponza madeejay wa uganda kwani wengi wao wanajidhalalisha kwa kuanika shida zao mitandaoni. Hata hivyo amedai kuwa aliwahi kuwa deejay kipindi cha nyuma na anafahamu kila kitu kuhusu hu-deejay, hivyo amewataka madeejay wa uganda kukoma kujiona wa maana kuliko watu wengine

Read More
 RAGGA DEE AWACHARUKIA WANAOKOSOA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021

RAGGA DEE AWACHARUKIA WANAOKOSOA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021

Msanii mkongwe kutoka Uganda Ragga Dee amezikingia kifua tuzo za Janzi Awards akisema tuzo hizo ni tofauti na tuzo ambazo tayari zimeandaliwa nchini Uganda. Tuzo hizo ambazo ziliandaliwa wiki hii iliyopita imekosolewa na baadhi ya wasanii kwa kukosa uwazi. Ragga dee amesema tuzo za Janzi zina dhamana kubwa ya takriban shillingi 112,998.26 za Kenya, hivyo mtu anaweza iuza na akapata pesa ambazo zimtasaidia kimaisha. Hitmaker huyo wa “Ndingida” amekanusha uvumi unaotembea mitandaoni kuwa kamati ya tuzo hizo ilipewa takriban shillingi millioni 28.6 kuandaa hafla hiyo kwa siku mbili akishangaa ni wapi walipata pesa hizo. Hata hivyo amedokeza kuwa watu ambao wamekuwa wakitoa lalama juu ya tuzo hizo ni wale ambao hawakushinda tuzo hata moja.

Read More