Rahmah Pinky afunguka chanzo cha kuondoka Team No Sleep

Rahmah Pinky afunguka chanzo cha kuondoka Team No Sleep

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Uganda Rahmah Pinky amevunja kimya chake juu ya kutengana na meneja wa vipaji, Jeff Kiwa. Pinky ameelezea kuwa Jeff Kiwa alipoteza mweelekeo kwenye suala la kusimamia muziki wake na akaanza kumtaka kimapenzi, jambo ambalo anadai hakuweza kulivumilia. “Mawazo yake yalibadilika na akaanza kutaka mambo mengine kutoka kwangu, ilibidi niikimbie lebo yake ya TNS kwa sababu sikutaka kukubali njia aliyotaka niifuate,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Kauli ya Pinky imekuja mara ya kudaiwa kuwa alitimuliwa kwenye lebo TNS inayoongozwa na Jeff Kiwa kwa kukosa nidhamu. Inaidaiwa kuwa licha ya kuonywa mara kwa mara kubadili mienendo yake, alipuuza ushauri wa uongozi wake na kuendelea kuvuta shisha huku akitoka kimapenzi na wanaume tofauti kwenye nyumba ambayo lebo ilimkodishia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake za kisanaa.

Read More
 MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AAPA KUVUNJA REKODI YA SHEEBAH KARUNGI

MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AAPA KUVUNJA REKODI YA SHEEBAH KARUNGI

Baada ya kuachia singo yake ya kwanza iitwayo “Superstar”, msanii mpya aliyechukua nafasi ya Sheebah Karungi kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep, Rahmah Pinky ameibuka na kujinasibu kuwa anaenda kuvunja rekodi ya Sheebah kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa kuachia hits kali bila kupoa. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 17 amesema atafanikisha hilo kupitia kipaji chake cha uandishi wa nyimbo na ukubwa wa uongozi wake. β€œSina ushindani na Sheebah, lakini nataka kufanikiwa zaidi kimuziki kuliko yeye. Nitatumia ujuzi wangu wa kuandika nyimbo kufanikisha hilo,” alisema katika mahojiano na runinga moja  nchini Uganda. Kadhalika, amesema atafanya kazi kwa bidii kama njia ya kumjengea msingi wa mashabiki ambao watamsaidia kupenya kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Hata hivyo Rahmah Pinky amesema kuwa anamheshimu sana Sheebah kama mtu ambaye alifungua milango kwa wasanii wengi wa kike nchini Uganda. Utakumbuka mwishoni mwa mwaka wa 2021 Sheebah Karungi aliigura lebo ya muziki ya Team No Sleep hii ni baada ya kuingia kwenye ugomvi wa mali na meneja wa Jeff Kiwa. Baada ya Sheebah kuondoka Jeff Kiwa alienda mbali zaidi na kumtambulisha Rahmah Pinky kama msanii mpya wa TNS kujaza pengo liloachwa na Hitmaker huyo wa Boy fire.

Read More