Ben Githae akerwa na wanaomkejeli baada ya mrengo wa Azimio la Umoja kupoteza uchaguzi

Ben Githae akerwa na wanaomkejeli baada ya mrengo wa Azimio la Umoja kupoteza uchaguzi

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Ben Githae ameonekana kuchukizwa na kitendo cha mashabiki kuendelea kumkejeli hata baada ya mrengo wa azimio la umoja kupoteza uchaguzi mkuu uliokamilika. Akizungumza kwenye hafla ya kuchangisha pesa huko Mlima Kenya, Githae amekiri kuumizwa sana na kauli ya watu wanaokumbusha kila mara namna mrengo aliokuwa anaunga mkono wa Azimio la umoja ulivyopoteza uchaguzi wa Agosti 9 huku akiwataka marafiki zake kumkubali kama mmoja wao badala ya kumsema vibaya kwa misingi ya kisiasa. Hitmaker huyo wa “Mabataro” amesema kwa sasa ameshakubali matukio kuwa muungano wa Azimio la umoja ulipoteza uchaguzi huku akisisitiza kuwa hana budi kukumbatia serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto. Miezi mitano iliyopita Ben Githae alikuwa gumzo nchini baada ya kuachia wimbo wa kisiasa uitwao “Kenya Is Safe”, wimbo ambao alikuwa anamsifia Raila Odinga kwa hatua ya kumchagua Martha Karua kama mgombea mwenza wa Azimio kwenye uchaguzi wa Agosti 9 ambapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa Kenya ipo salama mikononi mwa Odinga na Karua.

Read More
 MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

Mawakili wa Kinara wa ODM Raila Odinga na wale wa kundi la muziki la Sauti Sol wamekutana kwa ajili ya mazungumzo ili kutatua mgogoro wa hakimiliki ulioibuka mapema wiki hii baada ya wimbo wa Sauti Sol “Extravaganza” kupigwa kwenye mkutano wa Azimio. Wakili wa kundi la Sauti Sol, Moriasi Omambia ndiye amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter. “Ningependa kuthibitisha kwamba kundi linaloongoza kampeni za Raila Odinga na mawakili wao wanashirikiana nasi katika juhudi za kutatua mzozo uliopo kuhusu hakimiliki. Tunatambua kujitolea kwao katika kutafuta kusuluhisha jambo hili haraka iwezekanavyo.”  imesomeka tweet hiyo ya Omambia. Utakumbuka Chama cha ODM cha Raila Odinga kilitoa taarifa hapo awali kikisema kwamba walitumia muziki wa Sauti Sol kwa sababu wanapenda kazi za kundi hilo.

Read More