RALF RANGNICK ATANGAZWA KUWA KOCHA MKUU AUSTRIA
Shirikisho la soka nchini Austria limemtangaza rasmi Ralf Rangnick kama kocha mpya wa timu ya Taifa hilo kwa mkataba wa miaka miwili. Rangnick anachukua nafasi ya kuingoza timu ya Taifa kuanzia mwishoni mwa msimu huu hadi mwaka 2024. Hii haimaanishi kuwa ataachana na United hapana, Ralf ataendelea kuitumikia nafasi yake ya mshauri wa Manchester United kwa miaka miwili kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali. Hii ni fursa ya kuona soka la mtaalamu huyu wa 4-2-2-2 likifanya kazi akiwa kama kocha mkuu kuanzia msimu ujao.
Read More