Rapudo Amkingia Kifua Amber Ray Kufuatia Kashfa ya Obinna
Mfanyabiashara maarufu na mume wa sosholaiti Amber Ray,Kennedy Rapudo, amejitokeza hadharani kumtetea mkewe dhidi ya tuhuma alizoelekezewa na mwanahabari na mchekeshaji Oga Obinna. Kupitia video iliyosambazwa mitandaoni, Rapudo alieleza kutoridhishwa na jinsi Obinna alivyomkosoa Amber Ray hadharani. Rapudo alisema kuwa mke wake ni mwanamke anayejiheshimu na mchapakazi wa kweli, na kwamba hatakubali mtu yeyote kumvunjia heshima kwa misingi ya binafsi au ya kikazi. “Amber ni mke wangu na najua jinsi anavyojituma. Mtu yeyote anayemjua anajua kuwa anajiheshimu. Sitakubali mtu yeyote kumchafua hadharani,” alisema Rapudo kwa msisitizo. Kauli ya Rapudo ilikuja saa chache baada ya Oga Obinna kudai kuwa Amber Ray alifika kwenye shughuli ya kurekodi maadhui akiwa katika hali isiyofaa, akimtuhumu kuwa alikuwa amelewa kiasi na hivyo kuathiri utaratibu wa kazi. Obinna alidai kuwa hali hiyo ilisababisha ucheleweshaji na sintofahamu kazini. Amber Ray, kwa upande wake, alikanusha madai hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiyataja kama ya uongo na yenye lengo la kumharibia jina. Alisisitiza kuwa anajiheshimu na hajawahi kwenda kazini akiwa katika hali isiyo ya kitaaluma. Mvutano huu umeibua maoni tofauti miongoni mwa mashabiki wa burudani, huku baadhi wakiunga mkono msimamo wa Rapudo na Amber, na wengine wakitaka Obinna kutoa ushahidi wa madai yake au kuomba msamaha
Read More