Ray G akosa imani na chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA

Ray G akosa imani na chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA

Mwanamuziki Ray G amefunguka sababu za kutokuwa mwanachama wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Msanii huyo amesema chama hicho hakina mweelekeo lakini pia hajashawishika namna inawasaidia wasanii. Ray G ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Nobanza” amedai kwa sasa ana mpango wa kujiunga na UMA hadi pale atakapopata mwanga ya jinsi inatekeleza majukumu yake. Chama cha UMA katiika siku za hivi karibu kimepata pingamizi kutoka kwa wanamuziki mbali mbali nchini Uganda wengi wakidai kuwa hawaoni umuhimu wa chama hicho kwa kuwa imeshindwa kutetea maslahi ya wasanii.

Read More
 EX WA RAY G ADAI HAJUTII KITENDO CHA KUFURAHIA MSIBA ULIOMKUTA MSANII HUYO WA UGANDA

EX WA RAY G ADAI HAJUTII KITENDO CHA KUFURAHIA MSIBA ULIOMKUTA MSANII HUYO WA UGANDA

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Ray G, Elizabeth Namara amevunja kimya chake baada ya kuonekana akisherehekea kifo cha Binti wa msanii huyo. Kupitia video ya moja kwa moja iliyoweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Elizabeth Namara amethibitisha kuwa hajutii kitendo chake cha kufurahia msiba uliomkuta Ray G ambapo amewaonya wanaomkosa  waache kufuatilia na masaibu ya mahusiano yake kimapenzi. “Sitakata tamaa, nataka Ray G ateseke hadi pumzi yake ya mwisho. Nyinyi ambao mnahurumia mnapaswa kukoma kuingilia mambo ya watu zingatieni maisha yenu ya mahusiano. Hamuelewi ni jinsi gan Ray G aliniumiza,” alisema. Mrembo huyo amesema mwanamuziki huyo atalazimika kumuomba msamaha hadharani ikiwa anataka kuishi maisha ya furaha na familia yake. Ni kauli ambayo imeibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wamewashauri  Namara asamehe na asonge mbele na maisha yake. Itakumbukwa Ray G na mkewe, Annabelle, walimpoteza binti yao wa pili ambaye alizaliwa kabla ya wakati wake siku chache zilizopita, jambo ambalo lilimfanya mpenzi wake wa zamani, Elizabeth Namara kufurahia msiba alioupata. Kupitia ukurasa wake wa Facebook mrembo huyo alisema kwamba hatatulia hadi pale Ray G atakapolipa uharibifu aliyosababisha  katika maisha yake kwa kumpa ahadi za uongo kwamba atafunga ndoa naye.

Read More
 MWANAMUZIKI WA UGANDA RAY G AMPOTEZA BINTIYE WA SIKU 12

MWANAMUZIKI WA UGANDA RAY G AMPOTEZA BINTIYE WA SIKU 12

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ray G, ametangaza kumpoteza binti yake Kim aliyekuwa na umri wa siku 12. Kupitia mitandao yake ya kijamii Ray G , amesema mtoto huyo alifariki Disemba 21 kufuatia kusumbuliwa na ugumu wa kupumua. Msanii huyo amedokeza kwamba walifanya kila kitu kuokoa maisha ya binti yake huyo lakini juhudi zao ziliambuliwa patupu. Kim alikuwa mtoto wa pili kwa Ray G na alimpata na mrembo Annabell Twinomugisha.

Read More