Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Msanii wa R&B na mfanyabiashara Ray J ameibuka kwa hasira na kumshambulia vikali Suge Knight baada ya madai ya kushangaza aliyoyatoa kwenye kipindi cha televisheni cha Piers Morgan, ambapo Suge alisema kuwa Ray J na Diddy walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Madai haya yamezua hisia kali kwa Ray J na mashabiki wake. Ray J, ambaye awali alikuwa akimheshimu Rais huyo wa zamani wa Death Row Records, na kumtetea, alisema amevunjika moyo na kauli hizo zisizo na msingi. Alidai kuwa Suge amemshambulia kwa njia chafu na kuonyesha tabia ya kutojali, licha ya kuwa amekuwa akimuunga mkono katika nyakati ngumu. Aidha, Ray J alilalamikia namna Suge alivyoikosea heshima brand yake ya The Gaygency, inayosaidia wasanii wa jamii ya LGBTQIA+. Alisisitiza kuwa kuunga mkono jamii hiyo hakumaanishi kuwa yeye binafsi ni mpenzi wa jinsia moja, na ni aibu kwa Suge kutumia hilo kumshambulia. Ray J pia alimtuhumu Suge kuwa mtu anayeudhulumu watu wa karibu, ikiwemo wanaume na wanawake. Hadi sasa, Suge hajajibu madai hayo, huku mjadala ukiendelea kuenea mitandaoni kwa hisia kali kutoka kwa wafuasi wa pande zote.

Read More
 KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

Kanye West ameiambia Hollywood Unlocked kwamba alifanikiwa kuupata mkanda wa ngono kutoka kwa Ray J, ikiwa ni sehemu ya pili ya ule ambao ulivuja mwaka 2007 ukimuonesha Ray J na Kim Kardashian wakifanya mapenzi. Kwenye mahojiano ambayo ameyafanya na Hollywood Unlocked, YE amesema Kim alitokwa na machozi baada ya kufikishiwa mkanda huo. “Nilikwenda na kuchukua laptop mwenyewe kwa Ray J, na nilimpatia Kim Kardashian kwenye saa mbili asubuhi. Alilia sana baada ya kuona Laptop, unajua kwanini? Ni kwa sababu iliwakilisha namna gani watu walikuwa wanamtumia na kumchukulia kama bidhaa” alisema YE kwenye mahojiano hayo. Wack 100 aliyekuwa meneja wa Ray J ndiye alitusanua uwepo wa sehemu ya pili ya mkanda huo wa ngono. Masaa machache baada ya kutoka taarifa hiyo, upande wa Kim Kardashian umeibuka na kukanusha taarifa hiyo ikisema hakukuwa na maudhui yoyote ya ngono na hakuna sehemu ya pili ya mkanda huo. Aidha kwenye laptop hiyo kulikutwa video za Kim na Ray J wakiwa kwenye ndege wakielekea nchini Mexico na zingine wakiwa kwenye kumbi za starehe na migawaha.

Read More