RECHO REY AKANUSHA MADAI YA KUTOA UJA UZITO
Female Rapper kutoka nchini Uganda Recho Rey amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alitoa  uja uzito wake mwaka wa 2021. Katika mahojiano yake hivi karibuni Recho Rey amesema uvumi wa yeye kuavya mimba ulianza mara baada tumbo lake kupungua jambo ambalo amelikanusha kwa kusema kuwa hajawahi toa uja uzito wowote katika maisha yake ila kipindi hicho alikuwa anapitia changamoto nyingi katika maisha. Mrembo huyo amesema kuwa alipatwa na msongo wa mawazo kutokana na kuvulia kiuchumi hii ni baada ya uongozi wake kusitisha mkataba wa kusimamia muziki wake kipindi cha korona. Utakumbuka kwa sasa Recho Rey yupo mbioni kutafuta uongozi mwingine ambao utasimamia kazi zake za muziki.
Read More