RED BANTON AKANUSHA KUKWEPA KULIPA KODI

RED BANTON AKANUSHA KUKWEPA KULIPA KODI

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka Uganda Red Banton amekanusha tuhuma zinazosambaa mtandaoni kuwa amekuwa akikwepa kulipa kodi. Katika mahojiano yake hivi karibuni Red Banton amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwani ilikuwa ni njia ya wakosoaji wake kumchafulia jina. Aidha amesema tangu taarifa hizo zilipoibuliwa mtandaoni amefaidi pakubwa na pesa nyingi kutoka kwa wasamaria wema pamoja na marafiki zake wa karibu. Kauli ya Red Banton imekuja mara baada ya mwanamke mmoja mmiliki wa nyumba kuibuka na kumuanika Red Banton mtandaoni kwa kusema kwamba amekuwa akikwepa kulipa kodi ya nyumba anayoishi kwa muda mrefu baada ya kuingiwa na jeuri.

Read More