Remy Ma na Claressa Shields Warushiana Maneno Makali Kwenye Insta Story kisa Mwanaume

Remy Ma na Claressa Shields Warushiana Maneno Makali Kwenye Insta Story kisa Mwanaume

Rapa Remy Ma amemjibu Claressa Shields kupitia Insta Story, akimtaka akae kimya kuhusu uhusiano wake na Papoose. Katika ujumbe uliosheheni mafumbo, Remy alizungumzia mwanamke mwenye miaka 30 aliyeingia kwenye uhusiano na mwanaume mwenye miaka 47, mwenye historia ya ndoa ya muda mrefu na watoto wanne, huku akimuahidi mtoto mwingine na kuanza mchakato wa talaka saa chache zilizopita. Ujumbe huo umeeleweka kuwa umemlenga mwanamasumbwi Claressa. Hata hivyo haikuchukua muda, Clareesa Shields amemjibu Remy Ma kwa msimamo mkali, akisisitiza kuwa yeye na Papoose wana furaha, wanapanga familia, na hawamuogopi. Amemtaka Remy asaini talaka na kuheshimu maisha yao, huku wakijiandaa kwa tukio lao muhimu Julai 26. Hayo yote yameibuka baada ya Claressa kumtaja Papoose kwenye mahojiano na kusema bado hajamalizana rasmi na mke wake wa zamani. Remy alikanusha madai ya kutaka kurudiana na Papoose, akisisitiza kuwa talaka ilianza muda mrefu uliopita. Papoose naye alijibu kwa kuonyesha uthibitisho wa kuwasilisha talaka rasmi mahakamani, akisema alichelewa kwa sababu ya kumlinda binti yao dhidi ya drama ya umma. Drama hii ya ndoa ya mastaa hawa imechukua sura mpya, huku mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wakifuatilia kwa karibu na kutoa maoni mseto. Wengi wameelezea masikitiko yao kuona ndoa iliyowahi kusifiwa kama mfano wa mapenzi ya kweli ikivunjika hadharani.

Read More
 Remy Ma Asisitiza Kumaliza Ndoa Kwa Heshima, Aahidi Kumlipa Wakili wa Papoose

Remy Ma Asisitiza Kumaliza Ndoa Kwa Heshima, Aahidi Kumlipa Wakili wa Papoose

Msanii mashuhuri wa muziki wa hip hop, Remy Ma, amevunja ukimya wake kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na rapa mwenzake Papoose, akithibitisha kuwa bado mchakato wa talaka haujakamilika rasmi. Akizungumza kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye mtandao wa Instagram, Remy Ma alieleza kwa uwazi kuwa yuko tayari hata kugharamia ada za wakili wa Papoose ili kuhakikisha mchakato huo unakamilika kwa haraka na kwa utulivu. “Naweza hata kumlipia ada ya mwanasheria wake. Sitaki kuwa kikwazo katika maisha ya mtu,” alisema Remy kwa mtazamo wa amani na utu. Katika hatua nyingine, alijibu kauli za Claressa Shields, mpenzi wa sasa wa Papoose wakati wa mahojiano katika kipindi cha The Breakfast Club. Remy Ma alisema ingekuwa busara zaidi kwa Claressa kuomba mada hiyo kupuuzwa kwani ni ya faragha na bado iko kwenye mchakato wa kisheria. Alisisitiza kuwa hana chuki na hajawahi kuwa kikwazo kwa furaha ya Papoose. “Sijakasirika, wala sina chuki, lakini napenda kufafanua kuwa sina nia ya kumzuia Pap kupata furaha katika maisha yake. Sitaki simulizi za kupotosha ziendelee kusambazwa dhidi yangu,” alisisitiza. Kauli za Remy Ma zimepokelewa kwa mitazamo tofauti na wafuasi wake mitandaoni. Wengi wamepongeza namna alivyolishughulikia suala hilo kwa hekima na utu, huku wakisisitiza umuhimu wa watu kuachana kwa heshima bila kuzalishana visasi au migogoro isiyo ya lazima. Kwa sasa, mashabiki wa Remy Ma na Papoose wanasubiri kwa subira kuona hatima ya rasmi ya mchakato wa talaka hiyo, huku Remy akisisitiza kuwa lengo lake ni kuendeleza maisha kwa amani, bila kuathiri furaha ya mtu mwingine.

Read More