Baba yake Rihanna, Ronald Fenty, afariki dunia akiwa na miaka 70

Baba yake Rihanna, Ronald Fenty, afariki dunia akiwa na miaka 70

Ronald Fenty, baba mzazi wa nyota maarufu wa muziki wa pop Rihanna, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70. Kwa mujibu wa Starcom Network News kutoka Barbados, Fenty alifariki mapema Jumamosi asubuhi jijini Los Angeles baada ya kuugua kwa muda mfupi. Ingawa chanzo rasmi cha kifo chake hakijatangazwa, ripoti zinaeleza kuwa wanafamilia wake walikusanyika California kwa ajili ya kumuenzi na kuomboleza kifo chake. Hadi sasa, Rihanna hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu kifo cha baba yake. Taarifa za msiba huu zimekuja wakati Rihanna akiwa mjamzito na anatarajia mtoto wake wa tatu na mpenzi wake, rapa ASAP Rocky.

Read More
 Mchungaji aliyekufa na kufufuka, adai alikutana na watu wanateswa huku wimbo wa Rihanna ukipigwa

Mchungaji aliyekufa na kufufuka, adai alikutana na watu wanateswa huku wimbo wa Rihanna ukipigwa

Mchungaji mmoja Jijini Michigan Marekani ameibuka na kudai alikufa kwa muda na baada ya kufufuka ametusimulia mengi makubwa ya kustaajabisha. Mchungaji huyo kwa jina Gerald Johnson, ametumia mtandao wa TikTok kusimulia kwamba, baada ya kufa alienda kuzimu (Hell) na alikuta mashetani wakiwapa mateso makali binadamu ambao wametupwa huko motoni na kubwa la kushangaza ni kwamba, wimbo wa Rihanna “Umbrella” ulikuwa ukipigwa wakati mateso hayo yakiendelea. Johnson hakuamini kama angeenda kuzimu baada ya kufa ukizingatia alikuwa Mchungaji na alifanya mema ya kuwaweka binadamu kwenye mstari.

Read More
 Rihanna na Tems watajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo ya Oscar

Rihanna na Tems watajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo ya Oscar

Mwimbaji Temilade Openiyi a.k.a Tems kutoka Nigeria, ameweka Historia ya kuwa Msanii mwenye muda mfupi kwenye Muziki na kufanikiwa kutajwa kuwania Tuzo ya Oscar kupitia wimbo wa LiftMeUp alioshiriki kuuandika pamoja na Rihanna Licha ya Ukubwa wake kwenye tasnia ya Muziki, kwa mara ya kwanza Mwimbaji Rihanna naye amefanikiwa kuingia kwenye kipengele cha ‘Best Original Song’ kupitia wimbo wa Lift Me Up uliotumika kama Soundtrack ya Filamu ya Black Panther: WakandaForever Tems amefanikiwa kushinda Tuzo zaidi 30 na ametajwa kuwania zaidi ya Tuzo 80 hadi sasa. Rihanna amekuwa kwenye Muziki kwa takribani Miaka 18 na hadi sasa ana Tuzo 235 na kutajwa kuwania zaidi ya Tuzo 630. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Machi 12, mwaka 2023 huko Jijini Los Angeles nchini Marekani.

Read More
 Rihanna mbioni kuja na Documentary kuhusu maisha yake

Rihanna mbioni kuja na Documentary kuhusu maisha yake

Mwanamuziki Rihanna ameripotiwa kuwa anatengeneza Documentary kuhusu maisha yake kuelekea kwenye tukio kubwa la Super Bowl Halftime show ambayo atatumbuiza mwakani. Riri amesaini dili la mabilioni ya pesa na kampuni ya Apple, na vipande vya ‘Behind the Scenes’ vya Documentary hiyo vitarushwa. “Kuna hamu kubwa ya kufanya kila kitu na Rihanna, hasa kipindi hiki ambacho anarejea Jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.” chanzo kimoja kilieleza. Camera zitazunguka kuangazia maisha yake kama Mama mpya ambaye alijifungua mtoto mwezi Mei, akijitayarisha kwa ujio mpya kwenye muziki. “Atakuwa akirekodiwa wakati wa mazoezi (rehearsals) na vikao kuelekea usiku mkubwa wa onesho lake kwenye Halftime show ya Super Bowl. Hii ni kuonesha kwa undani maisha yake yalivyo.” chanzo kilieleza.

Read More
 Jina la mtoto wa Rihanna lazidi kuwaumiza Mashabiki vichwa

Jina la mtoto wa Rihanna lazidi kuwaumiza Mashabiki vichwa

Ni miezi mitano sasa imepita tangu Rihanna ajifungue mtoto wa Kiume, lakini hadi leo hajaanika wazi Jina la mtoto wala uso wake kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki zake wameanza kujiongeza na kulitafuta Jina la mtoto huyo hata kupitia mavazi ambayo anavaa Riri kwenye mitoko. Wikendi hii Riri alionekana akiwa amevaa cheni ndefu yenye herufi ‘D’ hivyo kuwafanya mashabiki zake wa nguvu kuhisi labda Jina la mtoto huyo linaanza na herufi hiyo. Kuna wengine ambao waliwahi kujiongeza na kudai Jina litakuwa linaanza na herufi ‘R’ kutokana na majina halisi ya Rihanna (Robyn) na A$AP Rocky (Rakim)

Read More
 VIDEO YA DIAMONDS YA RIHANNA YAWEKA REKODI YOUTUBE

VIDEO YA DIAMONDS YA RIHANNA YAWEKA REKODI YOUTUBE

Staa wa muziki duniani Rihanna ameweka rekodi kwenye mtandao wa YouTube licha ya kuwa nje ya muziki kwa takribani miaka 6 sasa. Video ya wimbo wake “Diamonds” imefikisha jumla ya views bilioni 2 kwenye mtandao huo. Ngoma hiyo iliachiwa rasmi Septemba 26, mwaka 2012 na video yake ilipakiwa kwenye mtandao wa YouTube Novemba 9, mwaka 2012. Diamond ni ngoma kutoka kwenye Album yake ya 7 (Unapologetic) ya mwaka 2012, na iliandikwa na Mwanamama Sia huku ikitayarishwa na Benny Blanco pamoja na Stargate.

Read More
 MREMBO AMINA MUADDI AKANUSHA KUVUNJA PENZI LA RIHANNA NA ASAP ROCKY

MREMBO AMINA MUADDI AKANUSHA KUVUNJA PENZI LA RIHANNA NA ASAP ROCKY

Mrembo mbunifu wa viatu Amina Muaddi ameibuka na kukanusha taarifa za kulivunja penzi la Rihanna na Asap Rocky. Kupitia insta stories kwenye mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameandika kwamba ameamua kufunguka kwa sababu taarifa hizo zinamvunjia heshima kwa kuwa Rihanna & A$AP Rocky ni watu ambao ana waheshimu kwa kiasi kikubwa sana. Kauli ya Mrembo huyo inakuja mara baada ya Mtu wa karibu na wawili hao kuuthibitishia mtandao wa TMZ kuwa stori za A$AP Rocky kumsaliti Rihanna na zile za kuachana hazina ukweli kwani wapenzi hao wako vizuri. Mapema jana ziliibuka stori hizo kupitia twitter na kusambaa kwenye mitandao yote duniani kwamba Riri ambaye ni mjamzito, ameachana na rapa AsapRocky mara baada ya kugundua kuwa anamsaliti kwa kutoka kimapenzi na mrembo mbunifu wa viatu kwenye kampuni ya Riri, Fenty aitwaye Amina Muaddi.

Read More
 TETESI ZA RIHANNA NA ASAP ROCKY ZASHIKA KASI MTANDAONI

TETESI ZA RIHANNA NA ASAP ROCKY ZASHIKA KASI MTANDAONI

Tetesi kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa mwanamuziki Rihanna amechana na mpenzi wake Asap Rock ambaye ndio baba mtoto wake mtarajiwa. Inadaiwa kuwa hii imetokana na Rihanna kumfumania mpenzi wake huyo akimsaliti na mmoja wa wabunifu wa viatu kutoka katika kampuni ya Fenty aitwaye Amina Mauddi. Tetesi hizo zinasema Asap Rocky na Amina Muaddi walianza mahusiano tangu mwezi Februari mwaka huu kwenye maonesho ya Paris Fashion Week. Taarifa hiyo imeenea kwa kasi kote mitandaoni haswa katika mtandao wa twitter baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao huo kuvujisha taarifa hiyo. Jambo lililoifanya idadi kubwa ya mashabiki na wafuatiliaji wa wapenzi hao kuanza kutiririsha maoni mbalimbali kuhusu jambo hilo. Baadhi ya vyanzo vimeonesha kuwa huenda kukawa na ukweli wa fununu hizi. Rihanna na Asap Rock siku za hivi karibuni wamekuwa wakiingia kwenye trending kama moja ya wapenzi wenye kuvutia zaidi baada ya wawili hao kuweka bayana kuwa wanatarajia kupata mtoto siku za usoni.

Read More
 RIHANNA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU UJA UZITO WAKE

RIHANNA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU UJA UZITO WAKE

Staa wa muziki kutoka marekani Rihanna amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ujauzito wake kwenye event yake ya Fenty Beauty Universe iliyofanyika Los Angeles Februari 11 mwaka huu. Akizungumza na Jarida la PEOPLE, Rihanna amefunguka kuhusu changamoto za kuwa mwanamitindo wakati akiwa mjamzito kwa kusema kuwa anafurahia kila hatua ya uja uzito wake na ndio maana anaacha tumbo lake wazi. Januari 31 mwaka huu Rihanna na AsAP Rocky walitangaza rasmi kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja kwa kuachia picha wakiwa matembezini mjini New York zilizomuonesha Riri akiwa mjamzito.

Read More
 NI RASMI SASA RIHANNA ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ASAP ROCKY

NI RASMI SASA RIHANNA ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ASAP ROCKY

Ni Rasmi sasa mwanamuziki kutoka nchini marekani Rihanna ni mjamzito. Mwimbaji huyo ambaye pia ni mwanamitindo anatarajia mtoto wake wa kwanza na rapa Asap Rocky. Tovuti mbali mbali za nchini Marekani zimeripoti taarifa hii kufuatia picha ambazo zimewaonesha wawili hao wakiwa matembezini mjini New York wikendi iliyopita. Mwaka 2019 ziliibuka taarifa kama hizi lakini alizikanusha kwenye mahojiano na Jarida la Vogue. ASAP Rocky na Rihanna wamekuwa marafiki wa karibu katika kipindi cha muda mrefu kabla ya kuthibitisha hadharani kuwa wanapendana mwaka wa 2021. Mwaka wa 2013, Rihanna alitokea katika video ya Asap Rocky ya “Fashion Killa” kama video vixen,jambo ambalo lilihusisha uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati yao.

Read More
 RIHANNA AANDIKA REKODI NYINGINE YOUTUBE, VIDEO YAKE YAFIKISHA VIEWS BILLIONI 1

RIHANNA AANDIKA REKODI NYINGINE YOUTUBE, VIDEO YAKE YAFIKISHA VIEWS BILLIONI 1

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rihanna anaelekea mwaka wa sita bila kuachia kazi yoyote ya muziki lakini kila siku anaweka rekodi. Rihanna ameandika rekodi nyingine kwa video yake “stay” kufikisha jumla ya views bilioni 1 kwenye mtandao wa youtube. Hii inamfanya rihanna kutanua rekodi yake ya kuwa msanii wa kike mwenye video nyingi zaidi zenye watazamaji zaidi ya bilioni kwenye mtandao wa youtube,kwani amefikisha jumla ya video 8 za muziki.

Read More