Ringtone awakosoa mapromota wa muziki wa Injili kwa kumlipa King Kaka shillingi laki mbili kwa show

Ringtone awakosoa mapromota wa muziki wa Injili kwa kumlipa King Kaka shillingi laki mbili kwa show

Mwanamuziki Ringtone Apoko ameamua kutoa ya moyoni, amewachana wadau wa muziki wa injili nchini DJ Moz na Njugush kwa kitendo cha kutowazingitia wasanii wa Gospel kwenye hafla ya mkesha wa mwaka mpya. Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Ringtone ameonesha kutofurahishwa na hatua ya wawili hao kumpa kipau mbele rapa King Kaka kwenye hafla hiyo ambayo kwa mujibu wake ilipaswa kuongozwa na wasanii wa nyimbo za injili. Hitmaker huyo wa “Omba” amesema kitendo cha msanii huyo wa kidunia kulipwa shilling laki mbili kutumbuiza kwenye shoo hiyo ambayo imefadhiliwa na hisani ni njia ya kuivunjia heshima tasnia ya muziki wa injili ikizingatiwa kuwa wasanii wengi wa gospel siku huyo hawakuwa na shughuli ya kufanya. “Maze nimejam,nimejam , nimejam sana,nimejam can you imagine ati King Kaka aliperform kwa event ya gospel akalipwa 200 thousand shillings na wasanii wa gospel siku hiyo walilala nyumbani hawana pahali pa kwenda kuimba!.,” Alisema kwenye video hiyo.

Read More
 Eric Omondi amjibu Ringtone kuhusu kazi ya Kshs. 50,000 kwa mwezi

Eric Omondi amjibu Ringtone kuhusu kazi ya Kshs. 50,000 kwa mwezi

Mchekeshaji Eric Omondi ameamua kumjibu Ringtone Apoko mara baada ya mwimbaji huyo kumkejeli kuwa ana mpango wa kumpa kazi ya shillingi Kshs.50,000 kwa mwezi. Kwenye mahojiano na Ankaliray katika kipindi cha Uhondo wa Milele FM, Omondi amesema hawezi kataa ofa ya kuajiriwa na Ringtone ila ana shauku ni wapi haswa mwimbaji huyo atatoa pesa za kumudu mshahara wake ikizingatiwa kuwa kodi ya nyumba anayoishi ni shillingi 45,000 kwa mwezi. Mchekeshaji huyo ameenda mbali na kudai kuwa Ringtone alifurushwa kwenye nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi mtaani Runda miezi sita iliyopita na sasa anaishi kwenye nyumba ya kupanga huko South C viungani mwa jiji la Nairobi. “Mimi kazi sijakataa, ila nyumba hata hana. Kwani hujui stori ya Ringtone. Nyumba ali auctioniwa. Anaishi South C- mi si najua kwake. Analipa aje 50,000 na rent yake ni 45,000.” Alisema Eric Omondi. Kauli ya Eric Omondi inakuja mara baada ya Ringtone kumtolea uvivu akiwa kwenye kipindi cha the Trend ya NTV ambapo alidai kuwa yupo tayari kumlipia mchekeshaji huyo shillingi 50,000 kwa mwezi kama mfanyikazi wake nyumbani ili aweze kumsaidia kufanya usafi kwenye mjengo wake wa kifahari huko mtaani Runda.

Read More
 “Niko tayari kumuajiri na kumlipa  Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

“Niko tayari kumuajiri na kumlipa Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko ameendelea kumuwashia moto mchekeshaji Eric Omondi baada ya kudai kuwa yuko tayari kumuajiri kama mfanyikazi wake wa nyumbani. Kwenye mahojiano na The Trend Ringtone amesema atamlipa Omondi shillingi millioni 50,000 kwa mwezi kwa kuwa amekuwa akiigiza kuishi maisha ya kifahari mtandaoni ambayo kwa mujibu wake hawezi kumudu. Katika hatua nyingine amemtolea uvivu mchekeshaji huyo kwa kusema kuwa hana kipaji cha ucheshi kwani amekuwa akitumia muda wake mwingi kukosoa shughuli za watu ili azungumziwe mtandaoni. Ringtone Apoko ambaye amekuwa akijinasibu kuwa msanii tajiri nchini Kenya, kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Ombi Langu” akiwa amewashirikisha wasanii wa kundi la Zabron Singers kutoka nchini Tanzania.

Read More
 Mashabiki wakoshwa na wimbo mpya wa Ringtone, wampa ushauri

Mashabiki wakoshwa na wimbo mpya wa Ringtone, wampa ushauri

Mwanamuziki Brown Mauzo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya baby mama wake Vera Sidika kukiri kufanya upasuaji wa kupunguza makali yake kutokana na matatizo ya kiafya. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika waraka mrefu akipongeza mrembo huyo kwa hatua ya kujitokeza wazi na kuweka mapungufu yake kwa umma huku akisema itakuwa funzo kwa wadada ambao kwa njia moja au nyinngine wataka kubadilisha miili yao kwa upasuaji. Katika hatua nyingine Mauzo amekiri kutamani maungo ya mrembo huyo kabla hajafanyiwa surgery ambapo ameenda mbali zaidu na kuhapa kwamba hatokuja kumkimbia Vera Sidika kutokana na muonekano wake mpya kwani alivutiwa na utu wake. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametafsiri ujumbe huo wa Brown Mauzo kuwa ni njia msanii huyo kutengeneza mazingira ya kuachia wimbo mpya huku wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa hatua vera sidika kutangaza hadharini kufanya upasuaji wa kupunguza makalio ilikuwa ni mkakati wa kumtoa kisanaa. Utakumbuka Brown mauzo na Vera Sidika ambaye walihalalisha mahusiano yao Septemba, 24 mwaka wa 2020 wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown.

Read More
 RINGTONE APOKO AWAPA SOMO WANAUME KUHUSU WANAWAKE WA KUOA

RINGTONE APOKO AWAPA SOMO WANAUME KUHUSU WANAWAKE WA KUOA

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko amezua mjadala mzito mtandaoni mara baada ya kutoa ushauri kwa wanaume ambao wapo mbioni kuingia kwenye ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone ame-posti picha ya pamoja ya William Ruto, Uhuru Kenyatta na wake zao na kusindikiza na caption inayowataka wanaume kuwaoa wanawake ambao ni wafupi kwa kimo kwa sababu wana nyota ya mafanikio kwenye maisha. Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” ameenda mbali zaidi na kuwaonya wanaume kutowachumbia wanawake warefu, akiwataja ni vizingiti kwenye masuala ya mafanikio. “PLEASE ALL MEN MARRY SHORT WOMEN IF U IS WANT TO MAKE IT AT YOUR LIFE PLEASE LEFT TALL WOMEN ALONE TALL WOMEN WILL STOLEN YOUR STAR ”, Ameandika. Kauli yake imeibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wametilia shaka uwezo wa kufikiria wa msanii huyo huku wengine wakimtaka arudi darasani kwa ajili ya kupata mafunzo fasaha ya lugha ya kiingereza.

Read More
 RINGTONE APOKO ATAJA KIASI CHA PESA ANAZOLIPISHA KWENYE SHOWS ZAKE

RINGTONE APOKO ATAJA KIASI CHA PESA ANAZOLIPISHA KWENYE SHOWS ZAKE

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone ameamua kutaja kiasi cha pesa anacholipisha kwa show zake  iwapo utahitaji kufanya kazi nae. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ringtonr ametangaza kuwa analipisha kwa show moja shillingi millioni 1 na shilling million 1.5 za Kenya kutokea kwenye klabu (Club Appearance). Ringtone ambaye juzi kati alitangaza kujiunga na muziki wa kidunia amesema amechukua hatua hiyo kutokana na mapromota kumhitaji sana  kwenye shughuli zao kwani amekuwa akitoa muziki mzuri. Lakini pia ametangaza kubadilisha jina lake la usanii kutoka kwa Ringtone kwenda kwa Blingtone huku akiri kuwa mapato ya nyimbo zake za Injili ambazo aliziimba kipindi cha nyuma itaenda kwa watoto mayatima. Ringtone amedokeza ujio wa ngoma yake mpya ambayo itaingia sokoni wiki hii ikiwa ni siku chache zimepita tangu atangaze kuanza kuimba nyimbo za mapenzi.

Read More
 ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Annastacia Mukabwa, amefunguka kwa mara ya kwanza baada msanii mwenzake Ringtone Apoko kutangaza kuacha muziki wa injili. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mukabwa amesema wimbo wake uitwao Kaa Kando ndio umempelekea Ringtone kuchukua maamuzi magumu ya kuacha muziki wa injili kwa sababu amekuwa akitumiwa na shetani kuichafua tasnia ya muziki huo nchini. “After releasing this Song Kaa Kando naona watu waliokuwa wamejificha ndani ya Gospel industry as Gospel artist wameanza kukaa Kando,” Amesema. “Wanatumiwa na shetani kuchafua sifa ya injili. Mungu anawaanika mmoja baada ya mwengine,” Ameongeza. Kauli yake imekuja mara baada ya Ringtone Apoko kudai kuwa wanawake waliokuwa wanamtaka kimapenzi ndio walimfanya akaacha muziki wa injili ambapo alienda mbali zaidi na kuwashauri wamfuate Yesu Kristo.  

Read More
 RINGTONE AWEKA WAZI SABABU ZA KUUKIMBIA MUZIKI WA INJILI

RINGTONE AWEKA WAZI SABABU ZA KUUKIMBIA MUZIKI WA INJILI

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo kutoka nchini Kenya Ringtone Apoko kwa mara ya kwanza ameamua kuweka wazi sababu za kuacha muziki wa injili. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ringtone amesema wanawake ndio walimpelekea kuchukua maamuziki magumu ya kuacha muziki wa injili na kugeukia muziki wa kidunia. Hitmaker huyo wa Sisi ndio Tuko ameenda mbali zaidi na kusema kwamba wanawake wengi nchini wamesusia kufuata Yesu Kristo na badala yake wameanza kumpenda kimapenzi jambo ambalo limemkatisha tamaa kwenye harakati zake za kusambaza injili kupitia nyimbo zake. Hata hivyo amesema ameamua kuchukua mapumziko mafupi kwenye muziki wake ili wanawake wanaomtaka kimapenzi wamwaache na kumrudia Yesu Kristo mwana wa Mungu. Kauli hiyo Ringtone imeibua maswali mengi miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa msanii huyo anatumia suala la kuacha muziki wa injili kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mitandaoni.

Read More
 MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI RINGTONE APOKO AWAPA SOMO WASANII WA KENYA

MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI RINGTONE APOKO AWAPA SOMO WASANII WA KENYA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone ametoa changomoto kwa wasanii wenzake kutotegemea waandaji wa matamasha kwa ajili ya kupata shoo za kuingizia kipato. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni ringtone amewataka wasanii nchini kutumia umaarufu wao kwa kuja na shoo zao wenyewe watakazofanya maeneo mbali mbali nchini kama njia ya kujikwamua kiuchumi. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pamela” amesema  wakenya wana moyo wa kuwasaidia wasanii wao lakini majivuno na kiburi imewaponza wasanii wengi  na hivyo kuwafanya kukosa ubunifu wa kugeuza muziki wao kuwa biashara. Utakumbuka mwaka wa 2010 Ringtone alianzisha mpango wa kutembelea shule zote za upili nchini kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wanafunzi kuhusu masuala yanayowaathiri ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwapa burudani na kuuza kanda za nyimbo zake jambo ambalo lilimuingizia pesa nyingi.

Read More