“Nilikuwa Nakojoa Kitandani Nilipokuwa Nikimchumbia Mume Wangu” – Risper Faith Afunguka Bila Woga
Mrembo na mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Risper Faith, ameacha wengi midomo wazi baada ya kufichua siri ya kushangaza kuhusu kipindi cha uchumba wake na mumewe. Kupitia mahojiano ya moja kwa moja kwenye mtandao wa YouTube, Risper alikiri kuwa alipokuwa akichumbiana na mumewe, alikuwa akijikojolea kitandani mara kwa mara. Katika maneno yake yaliyowavutia wengi mitandaoni, Risper alisema kwa ujasiri: “When I was dating my husband, nilikuwa nakojoa kwa kitanda. Not most of the time, like twice a week.” Kauli hiyo imeibua hisia tofauti mitandaoni baadhi wakishangazwa na ujasiri wake wa kufichua jambo linalochukuliwa kuwa la aibu, huku wengine wakimpongeza kwa kuwa mkweli na wazi kuhusu maisha halisi ya mwanadamu. Risper Faith, ambaye alipata umaarufu kupitia reality show ya Nairobi Diaries, ni mmoja wa watu mashuhuri wanaoamini katika kuishi maisha halisi ya kutoigiza. Mara kwa mara amekuwa akizungumza kuhusu mabadiliko ya mwili wake, ndoa, changamoto za uzazi, na maisha ya kifamilia jambo linalomletea mashabiki waaminifu na wakati mwingine, wakosoaji wakali. Kauli yake kuhusu kukojoa kitandani ni mwendelezo wa mtindo wake wa kuwa wazi bila uoga, na huenda ikawa ni chachu kwa wengine kuelewa kuwa hali kama hizo hazipaswi kufichwa kwa aibu bali kueleweka na kusaidiwa.
Read More