SPICE DIANA AZIDI KUMUANDAMA PROMOTA MUTIMA KISA DENI

SPICE DIANA AZIDI KUMUANDAMA PROMOTA MUTIMA KISA DENI

Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana ameonesha kusikitishwa na hatua ya promota Robert Mutima kukataa kumlipa pesa zake zilizosalia baada ya kutumbuiza kwenye show ya promota huyo huko Masaka. Mrembo huyo amesema licha ya promota huyo kuahidi kumlipa pesa hizo kwa wakati hadi sasa hajatimiza ahadi yake hiyo ambapo amehapa kuwa ataendelea na harakati ya kumshinikiza amlipe haki yake. Utakumbuka mwezi uliopita Spice Diana alikamata vichwa vya habari nchini Uganda alipomkashifu Mutima hadharani akiwa jukwaani baada ya kushindwa kulipa pesa zake, lakini wawili hao walikuja wakakutana ambapo promota huyo aliomba radhi na kuahidi kumlipa.

Read More
 PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Siku chache baada ya Promota Robert Mutima kumuomba radhi msanii Spice Diana kwa kuchelewesha pesa zake, promota huyo ameibuka tena kumchana msanii huyo kwa kitendo cha kumuahibisha mbele ya mashabiki zake. Mutima amesema alishangazwa na kitendo Spice Diana na huenda mrembo huyo anatumia mihadarati kabla ya kupanda jukwaani kwani njia ambayo alitumia kudai haki yake haikuwa nzuri. Amesisitiza kuwa alikuwa ameshikika na majukumu mengine ambayo yalimkwamisha kutofika kwa wakati kwenye shoo hiyo kukamilisha malipo ya msanii Spice Diana. Utakumbuka baada ya Spice Diana kusimamisha performance yake huko Masaka nchini Uganda alimtuhumu Mutima kwa kutokuwa mwazi kwenye ishu ya malipo ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka mashabiki wabebe vifaa vyote vya kielektroniki kama njia ya kumuadhibu promota huyo jeuri.

Read More
 PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

Promota wa muziki kutoka Uganda Robert Mutima amemuomba msamaha msanii Spice Diana baada ya kushindwa kumlipa pesa zake. Katika taarifa promota huyo amekiri kumvunjia heshima mrembo huyo kwa kusema kwamba hakuweza kumlipa kwa wakati kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake. Hata hivyo Spice Diana amepokea msamaha wa promota huyo kwa mikono miwili huku akisema hana kinyongo naye ila alikuwa anadai haki yake. Wikiendi iliyopita, mashabiki waliachwa na mshangao baada ya Spice Diana kusimamisha show yake ghafla huko Masaka ambapo alianza kumsomea Robert Mutima akitaka amlipe pesa zake.

Read More