ASLAY, ABBY CHAMS NA YOUNG LUNYA WASAINIWA ROCKSTAR AFRICA
Label ya Rockstar Africa imetangaza rasmi kuwasaini wasanii watatu kutoka nchini Tanzania; Young Lunya, Abby Chams na Aslay. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, label hiyo imewakaribisha kwenye familia yao ambayo pia inafanya kazi na mkali Ommy Dimpoz. Rockstar Africa ni label inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment na ilianzishwa mwaka 2015 na Mtanzania Christine βSevenβ Mosha ambaye ndiye muanzilishi na mmiliki. Label hiyo ishawahi kufanya kazi na wasanii kama Ali Kiba, Lady Jay Dee na Baraka The Prince.
Read More