DJ Romy Jons Amjibu Lava Lava Kuhusu Malalamiko ya Kufanyiwa Fitina

DJ Romy Jons Amjibu Lava Lava Kuhusu Malalamiko ya Kufanyiwa Fitina

Dj maarufu kutokaTanzania, Romy Jons maarufu Dj RJ, ameibua gumzo baada ya kutoa maoni yake kuhusu malalamiko ya msanii wa Bongo Fleva, Lava Lava. Hii ni baada ya Lava Lava mapema jana kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba yeye ndiye msanii anayeongoza kwa kufanyiwa fitina kila anapotoa kazi mpya. Kupitia maoni yake kwenye posti hiyo, Dj RJ alimjibu moja kwa moja kwa kusema kuwa Lava Lava hafanyii fitina bali ukweli ni kwamba nyimbo zake si kali kiasi cha kutikisa sanaa. Aliendelea kumshauri msanii huyo kutafuta mtu wa kumwandikia mashairi, akibainisha kuwa wasanii wengi wakubwa wamekuwa wakifanya hivyo ili kuboresha kazi zao. Kauli ya Dj RJ imeibua mitazamo tofauti mitandaoni. Wapo waliokubaliana naye wakisema ushauri huo ni wa kweli na unaweza kusaidia Lava Lava kufikia viwango vikubwa zaidi, huku wengine wakimtetea Lava Lava wakidai changamoto anazokumbana nazo ni za kimfumo na zinahusisha chuki binafsi kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzake. Mjadala huu umeendelea kushika kasi, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Lava Lava atajibu moja kwa moja ushauri huo au ataendelea kusimamia msimamo wake kuhusu kufanyiwa fitina.

Read More
 Khadija Kopa achukizwa na ujumbe wa kaka yake Diamond

Khadija Kopa achukizwa na ujumbe wa kaka yake Diamond

Malikia wa mipasho Tanzania Khadija Kopa ambaye pia ni mama mzazi wa nyota wa muziki wa bongo fleva Zuchu, ameonesha kuchukizwa na ‘Komenti’ ya Romy Jons ambayo aliiandika kwenye ukurasa wa Instagram wa Zuchu. ‘Komenti’ hiyo iliandikwa baada ya Zuchu kuposti picha zake akita amevaa ‘Taiti fupi’, Romi aliandika, ‘’SHAPE NDIO HUNA MWAYA’. Kupitia ‘komenti’ hiyo Khadija Kopa alishindwa kuvumilia na kuamua kutoa neno kumtaka Mwanae asiende Uturuki ambapo wengi huwa wanaenda kufanya upasuaji ili kuongeza umbo. Khadija aliandika, ‘’Wala usiende Uturuki mwanangu alonacho yeye huna na ulonacho wewe yeye hana huyo ndio Mungu @romyjons’’ Ikumbukwe kuwa Romy amekuwa mtu wa utani mwingi katika mitandao ya kijamii hasa katika komenti zake ambazo huwa anaandika kwa baadhi ya kurasa za watu mbalimbali.

Read More
 RJ THE DJ ARUSHA JIWE GIZANI, AWACHANA WALIOMDHARAU DIAMOND PLATINUMZ

RJ THE DJ ARUSHA JIWE GIZANI, AWACHANA WALIOMDHARAU DIAMOND PLATINUMZ

DJ wa Diamond Platinumz ambaye pia ni Kaka wa bosi huyo wa WCB Romy Jons amewataka watu wapendane hata kama mtu hana mbele wala nyuma Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Romy Jons amewataka watu wathaminiane ujumbe uliomaanisha kuwa hakuna aijuaye kesho yako au yake. “Kuna baadhi ya ndugu/marafiki walimdharau sana na kumkebehi mdogo wangu nasibu, hakuna alieamini katika ndoto yake, leo ndio hao mstari wa mbele kuomba msaada, tupendane na kuthaminiana hata kama hatuna mbele wala nyuma”. Ameandika kwenye Istagram yake. Hii inakuja mara baada ya watu waliomdharau mdogo wake Diamond Platnumz kwa kutoamini katika ndoto yake kipindi cha nyuma lakini leo wamekuwa mstari wa mbele kwenye suala la kumuomba msaada.

Read More