Ronald Alimpa akiri kuacha kutumia dawa za kulevya

Ronald Alimpa akiri kuacha kutumia dawa za kulevya

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ronald Alimpa amekiri kuwa amekuwa akitumia mihadarati kama wasanii wengine duniani. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni anasema wakati huo alikuwa akivuta bangi na hakuna mtu ambaye angemzuia kufanya chochote alichotaka kwani hakuwa amekumbana na madhara ya kutumia dawa za kulevya. Hata hivyo, Ronald Alimpa amethibitisha kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya kulazwa hospitalini kufuatia kunusurika kwenye ajali mbaya ya barabarani. Msanii huyo anasema maumivu aliyokuwa nayo wakati wa operesheni yalikuwa makali, hivyo madaktari walimshauri aachane na dawa za kulevya kwani huenda ingeathiri maisha yake siku za mbeleni. Katika hatua nyingine Alimpa amefichua ujio wa wimbo wake mpya uitwao  “Onyenyangamu” ambao utaingia sokoni hivi karibuni. Anasema wimbo wake mpya unauachia kwa ajili ya kusherehekea uhai wake na pia kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha kwani nusra aage dunia alipohusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Read More
 Ronald Alimpa akamatwa kwa kususia show

Ronald Alimpa akamatwa kwa kususia show

Msanii kutoka nchini Uganda Ronald Alimpa ameripotiwa kukamatwa kufuatia hatua ya kususia show zake tatu ambazo alipaswa kutumbuizwa Disemba 25 na 26 mtawalia. Kushindwa kwake kutumbuiza kwenye show hiyo kuliwafanya mashabiki wenye ghadhabu waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, kuharibu mali ya mamillioni ya fedha iliyowaacha mapromota wakikadiria hasara kubwa. Hitmaker huyo wa “Seen Don” ambaye amekuwa akiuguza majeraha ya ajali aliyoipata miezi kadhaa iliyopita,alipaswa kutumbuiza kwenye show hiyo akiwa kwenye kiti cha magurudumu kutokana na kupoteza miguu yake katika ajali hiyo. Kwa sasa tunasubiri tamko la meneja wa Ronald Alimpa kunyoosha maelezo juu ya msala wa kukamatwa kwake lakini pia chanzo cha kutofika kwenye eneo la show kwa wakati licha ya kulipwa pesa zote.

Read More
 Meneja wa muziki nchini Uganda James Mulwana afunguka kuvunja mkataba na msanii Ronald Alimpa

Meneja wa muziki nchini Uganda James Mulwana afunguka kuvunja mkataba na msanii Ronald Alimpa

Misala haiishi kwa msanii Ronald Alimpa kutoka nchini Uganda, 2022 unakuwa mwaka mbaya kwake. Baada ya msala wa ajali ya barabarani uliompelekea kulazwa hospitalini, sasa ni zamu ya meneja wake James Mulwana. Mulwana ambaye amekuwa akimsimamia kimuziki ametangaza kuvunja mkataba na msanii huyo kutokana na tabia yake ya utukutu. Katika mahojiano yake hivi karibuni meneja huyo wa muziki amesema anasubiri Alimpa apate nafuu kutokana na majeraha mabaya aliyopata kwenye ajali ya barabarani mwezi mmoja uliopita kisha atasitisha utoaji wa huduma kwa msanii huyo. “We had parted ways but I came back when he got into an accident. With his current attitude, I can’t continue with him. I will finalize our business this month,” Alisema Mulwana Kauli ya James Mulwana imekuja mara baada ya Hitmaker huyo wa “Seen don” kumporomoshea matusi ya nguoni mama yake mzazi kwa hatua ya kutumia vibaya pesa alizochangiwa na wahisani kugharamia matibabu yake hospitalini. Aidha, baada ya Alimpa kumvunjia heshima mama yake mzazi, mganga wa kienyeji nchini Uganda Mama Fina ambaye amekuwa akimsaidia msanii huyo kifedha aliamua pia kusitisha kutoa huduma kwake.

Read More
 Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mganga wa kienyeji kutoka nchini Uganda Mama Fina ameamua kumkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga baada ya kutuhumiwa kuhusika kwenye wizi wa pesa za kugharamia matibabu ya msanii Ronald Alimpa aliyehusika kwenye ajali mbaya ya barabarani wiki iliyopita. Mama Fina amenyosha maelezo kwa kusema kuwa hakumpa Hassan Nduga pesa za Ronald Alimpa kama inavyodaiwa bali alitoa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya msanii huyo na akampa mama yake mzazi. Mwanamama huyo amesisitiza kuwa bado anaendelea kumtumia pesa za mahitaji ya msingi msanii huyo ambaye bado anauguza majeraha mabaya ya ajali. Kauli ya Mama Fina inakuja baada ya familia ya Ronald Alimpa kumchafulia jina Hassan Nduga kwa madai ya wizi wa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya hitmaker huyo wa “Seen Don” alizopewa na mama Fina.

Read More
 Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Msanii kutoka nchni Uganda Ronald Alimpa ameonesha kusikitishwa na kitendo cha msanii mwenzake Hassan Nduga kuhusika kwenye wizi wa pesa za msaada alizopewa na wahisani kwa ajili ya kugharamia matibabu yake. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Alimpa amesema  msanii huyo alifuja takriban shillingi millioni 1.5 kati ya millioni 2 alizopokea kutoka kwa msamaria mwema kwa kigezo cha kugharamia mahitaji ya wasanii wenzake waliopata naye ajali wiki moja iliyopita. Hitmaker huyo huyo “Alimpa” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya Nduga kumsaidia kipindi alihusika kwenye ajali ya barabarani hajafurahishwa na kitendo chake cha kuwatangazia watu misaada aliyokuwa anampa akiwa hospitalini. Utakumbuka Ronald Alimpa, Lady Grace na Ragga Fire walihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani huko Ssemuto Katika wiliya ya Nasakeseke wiki moja iliyopita, lakini kwa bahati mbaya  msanii lady grace alifariki dunia papo hapo huku akiwaacha wengine na majeraha mabaya.

Read More
 Wahisani waridhia ombi la kumsaidia Ronald Alimpa baada ya kuhusika kwenye ajali

Wahisani waridhia ombi la kumsaidia Ronald Alimpa baada ya kuhusika kwenye ajali

Wahisani wameridhia ombi la kumsaidia msanii kutoka Uganda Ronald Alimpa aliyehusika kwenye ajali mbaya barabarani Septemba 29 mwaka huu. Kwa mujibu wa picha zinazosambaa mtandaoni, Hitmaker huyo wa “Seen Don” anaendelea kupokea msaada wa kifedha na mahitaji mengine ya msingi kutoka kwa wasanii wenzake, mashabiki pamoja na marafiki huku akiwa anauguza majeraha mabaya kwenye hospitali moja jijini Kampala. Hatua hii imekuja siku mbili baada ya msanii huyo kupitia video iliyosambaa mtandaoni kuwaomba wahisani kuchangisha fedha za kugharamia matibabu yake.

Read More
 Mwanamuziki Ronald Alimpa aomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki Ronald Alimpa aomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa anaomba msaada wa kifedha baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani Septemba 29 mwaka huu. Kwenye video inayosambaa mtandaoni alimpa ambaye amelazwa hospitalini amewaomba mashabiki, wanafamilia, marafiki na wahisani kumchangishia pesa ili aweze kulipa gharama ya matibabu. Ronald Alimpa na msanii Lady Grace na Ragga Fire walihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani huko Ssemuto Katika wiliya ya Nasakeseke jana Alhamisi. Lakini kwa bahati mbaya  msanii lady grace alifariki dunia papo hapo huku akiwaacha wengine na majeraha mabaya.

Read More
 RONALD ALIMPA AKANUSHA KUIBA WIMBO WA KABAKA ATUMYE

RONALD ALIMPA AKANUSHA KUIBA WIMBO WA KABAKA ATUMYE

Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa amekanusha tuhuma za wizi wa wimbo wa wa kabaka Atumye zilizoibuliwa na msanii mwenzake Baby J. Katika mahojiano yake hivi Alimpa amesema ameshangaza na hatua ya Baby J kudai kuwa aliiba ubunifu wa wimbo wake wa Kabaka Atumye na kuutumia kwenye wimbo wake mpya bila ridhaa yake. Hitmaker huyo wa Seen Don amesema aliandikiwa wimbo huo na uongozi wake hivyo hakujua kama kuna wimbo wa  Baby J ambao una jina sawa na wake. Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yuko tayari kukutana na Baby J kwa ajili ya kutatua  tofauti zao. Utakumbuka mwaka wa 2017 Baby J aliachia wimbo uitwao kabaka Atumye chini ya Climax Records lakini wimbo huo haukupokelewa vyema na wapenzi wa muziki mzuri  nchini Uganda kama ilivyo kwa tolea la Ronald Alimpa.

Read More
 RONALD ALIMPA AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYAA

RONALD ALIMPA AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYAA

Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa mraibu wa dawa za kulevya. Katika mahojiano yake hivi karibuni Alimpa amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa hatumii kabisa mihadarati katika maisha yake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Seen Don” amesema madai hayo yameibuliwa na watu wenye nia ya kumpaka tope huku akikiri mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa mwaka wa 2016 lakini kilichomkuta kilimfanya achane na matumizi ya dawa hizo. Kauli ya Ronald Alimpa imekuja mara baada ya promata mmoja nchini Uganda kudai msanii huyo alimdhalilisha kwa kumpulizia moshi ya bangi usoni walipomteka nyara pamoja na timu yake kufuatia mzozo uliobuka kati yao aliposusia kutumbuiza kwenye shoo yake.

Read More