Rosa Ree kuachia album yake mpya mwishoni mwa mwezi Novemba

Rosa Ree kuachia album yake mpya mwishoni mwa mwezi Novemba

Rapa wa kike kutoka Tanzania Rosa Ree ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya iitwayo “Goddess” ambayo ameitaja kuiandaa kwa takribani miaka minne. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amebainisha kwamba, anaachia album yake hiyo kama msanii anayejitegemea mwenyewe yani adhaminiwi na lebo yoyote na wala hajauza muziki wake kwa kampuni yoyote ya usambazaji wa muziki. Hitmaker huyo wa “Watatubu” amesema kampuni nyingi zilimfuata kutaka kumdhamini lakini amesema amechagua kumiliki muziki wake kwa asilimia mia. Hata hivyo ameeleza kuwa albamu yake hiyo itaingia sokoni Novemba 26 mwaka huu,  huku akisema album ya Goddess ina aina mbalimbali za muziki ambazo zinamtambulisha yeye ni nani hasa.

Read More
 ROSA REE AFUTA PICHA ZA MPENZI WAKE PETROUSSE INSTAGRAM

ROSA REE AFUTA PICHA ZA MPENZI WAKE PETROUSSE INSTAGRAM

Msanii wa Bongofleva, Rosa Ree amefuta picha zote za mchumba wake, King Petrousse katika ukurasa wake wa Instagram. Hatua hiyo inakuja mara baada ya miezi hivi karibuni Rosa Ree kutokuonekana kuposti sana picha za King Petrousse kama ilivyokuwa hapo awali. King Petrousse alimvisha Rose Ree pete ya uchumba Septemba mwaka jana, kisha kwenda Zanzibar kwa ajili ya mapunziko. Utakumbuka baada ya hatua hiyo, King Petrousse alioneka kwenye video ya wimbo wa Rosa Ree, Mulla akimshirikisha Abby Chams iliyotoka Desemba 2022.

Read More
 ROSE REE AFUNGUKA KUSAINIWA NA RICK ROSS

ROSE REE AFUNGUKA KUSAINIWA NA RICK ROSS

Msanii wa muziki Bongofleva, Rosa Ree amefunguka kuhusu kusainiwa kwenye lebo ya Rick Ross, Maybach Music Group. Akizungumza na XXL ya Clouds FM, Rosa Ree amesema anafurahia kuona Rick Ross kakubali muziki wake na mambo yatakapokuwa tayari mashabiki wake tafahamu. “Kiukweli nashukuru kuona Rick Ross mtu ambaye nimekuwa nikimsikiliza tangia nipo shule anakuwa anakubali kitu ambacho nakifanya, hata nilipotoa wimbo wangu wa mwisho, Blueprint alitoa maoni kwamba ni kitu kizuri”. “Mambo ni mazuri kwa sababu tunawasiliana, tunaongea na huwezi kujua yajayo yanaweza kuwa ni makubwa sana, sitaki kufichua chochote napenda mfahamu ni kitu gani kitakuwepo huko mbele pindi tutakapokuwa tayari” alisema Rosa Ree. Ikumbukwe toka ameanza muziki Rosa Ree amepita kwenye lebo kama The Industry na Dimo Production ya Afrika Kusini.

Read More
 ROSA REE AFUNGA NDOA YA SIRI NA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU

ROSA REE AFUNGA NDOA YA SIRI NA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU

Female rapper kutoka nchini Tanzania Rosa Ree amethibitisha kufunga ndoa ya kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu alie mtambulisha kama King Petrousse huko Moshi, Kilimanjaro.. Rosa Ree ametumia ukurasa wake wa Instagram kushare mfululizo wa picha zenye ujumbe unaoashiria kuwa sasa ameingia rasmi kwenye ndoa akiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni yanayovaliwa kwenye ndoa za Kinyarwanda, ‘Umushanana. Picha hizo za Rosa Ree na mpenzi wake Petrouse imeibua hisia za mashabiki wake na mastaa wenzake ambao wameenda mbali na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani. Ikumbukwe Rapper huyo na mchumba wake wa tangia wakisoma shule ya sekondari, king petrousse wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka mitano na waliweka wazi mahusiano yao kwa umma mwezi Septemba mwaka huu.

Read More