Rose Muhando Awapuuza Wanaume Wanaomtaka Kimapenzi
Msanii wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Rose Muhando, ameweka wazi msimamo wake kuhusu masuala ya mahusiano na ndoa, akisisitiza kuwa hawezi kukubali ombi lolote la mwanaume anayemtaka kimapenzi bila kupata ruhusa kutoka kwa Mungu. Akizungumza kwenye podcast ya Sky Walker, Rose amesema maamuzi yote makubwa katika maisha yake huongozwa na imani, na suala la mapenzi haliko tofauti. Kwa mujibu wake, hata mwanaume akionyesha mapenzi ya dhati, kujitoa kwa kiwango kikubwa au hata kulia, bila ridhaa ya Mungu hawezi kufanya uamuzi wa kuingia kwenye mahusiano. Kauli yake imekuja mara baada ya kukiri kuwa ni kweli pasta wa Kenya aliwahi kuwasilisha ombi la kumtaka kimapenzi, lakini alimjibu kwa utulivu na hekima kwamba bado anasubiri majibu kutoka kwa Mungu kabla ya kufanya uamuzi wowote.
Read More