Rufftone afunguka sababu za kumchumbi mke wake kwa zaidi ya miaka 8

Rufftone afunguka sababu za kumchumbi mke wake kwa zaidi ya miaka 8

Msaniii mkongwe kwenye muziki nchini Rufftone amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu hatua ya kumchumbia mke wake Crystal kwa zaidi ya miaka 8. Kwenye mahojiano na Plug TV rufftone amesema kipindi hicho alikuwa ameshikika na masuala ya muziki lakini pa alikuwa na marafiki wengi wa kiume kiasi cha kumfanya kusahau  kuingia kwenye maisha ya ndoa. Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” amesema aliogopa sana kuingia kwenye ndoa kwa sababu alikuwa anahisi mke angemnyima uhuru wa kutangamana na marafiki zake lakini baada ya kuhamua kuoa alikuja akagundua alipoteza muda mwingi kuwa na mitazamo hasi huu ya ndoa. Lakini pia amewataka wasanii wa injili waliogeukia kufanya muziki wa kiduani kutubu na kurudi kumtukia mwenyezi mungu ikizingatiwa kuwa bado wana nafasi nyingine ya kuwaburudisha mashabiki zao . Hata hivyo amemkataa hadharani msanii Ringtone Apoko ambaye amekuwa akijiita mwenyekiti wa muziki wa injili nchini kwa kusema kuwa sio vibaya msanii kujitawaza jina hilo lakini kwa upande wake yeye anahisi Yesu pekee ndiye anastahili kushikilia wadhfa huo.

Read More
 RUFFTONE AZUA GUMZO MTANDAONI, AIBUA TUHUMA NZITO DHIDI YA DADDY OWEN

RUFFTONE AZUA GUMZO MTANDAONI, AIBUA TUHUMA NZITO DHIDI YA DADDY OWEN

Mgombea wa wadhfa wa useneta kaunti ya Nairobi msanii Rufftone amezua gumzo mtandaoni mara baada kuibuia madai mazito dhidi ya kaka yake Daddy Owen. Akiwa kwenye moja ya interview Rufftone amesema miaka kadhaa iliyopita Daddy Owen ambaye kwa wakati huo alikuwa mfuasi sugu wa Chama ODM alimkimbiza kwa panga nusra amkatekate na tangia kipindi hicho hajawahi kipenda chama hicho kwani anakihusisha na uhuni. Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” alishindwa kueleza kwa kina mfumo wa uchumi wa bottom up ambao unaendesha na chama cha UDA  ambacho kinaongozwa na Naibu wa rais Dkt William Ruto. Hata hivyo ametoa wito kwa wakenya kuwachagua viongozi vijana ambao watabadilisha taifa  hili kwa kuleta maendeleo mashinani.

Read More