RUTH MATETE AWAONYA WANAWAKE DHIDI YA KUWATONGOZA WANAUME

RUTH MATETE AWAONYA WANAWAKE DHIDI YA KUWATONGOZA WANAUME

Mwimbaji wa nyimbo za injili aliyegeukia ukasisi Ruth Matete amewaonya wanawake dhidi ya kutongoza wanaume. Kwenye mahojiano na Lupaso TV, Matete amesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na maandiko matakatifu lakini pia ni kuidhalilisha jinsia ya kike. Kulingana na mama huyo wa mtoto mmoja, wanaume ndio wanapaswa kuwa wa kwanza kuwatokea au kuwatongoza wanawake na sio vinginevyo. Mwimbaji huyo amewashauri wanawake kumgeukia Mungu kwenye suala la kumtafuta mume mwema atakayekidhi matamanio yao badala ya kwenda kinyume na itakidi za kijamii. Hata hivyo amefichua kuwa yupo single na anatafuta mwanaume wa ndoto yake ambaye anamzidi kiumri kwani ni watu ambao wana malengo kwenye maisha. Utakumbuka Ruth Matete alijipata kwenye njia panda baada ya kumpoteza mume wake John Apewajoye kwenye ajali ya moto mwaka 2020. Hata hivyo baada ya mume wake kufariki watu walimshambulia mitandaoni wakidai huenda alihusika moja kwa moja kwenye kifo cha mume wake huyo madai ambayo aliyekana.

Read More
 RUTH MATETE AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUINGIA KWENYE NDOA

RUTH MATETE AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUINGIA KWENYE NDOA

Msaniii Ruth Matete amefunguka kuhusu suala la kuingia kwenye mahusiano mengine. Kupitia Instagram mama huyo wa mtoto mmoja amesema hivi karibuni atafikisha umri wa miaka 40 na anatamani kupata watoto zaidi ya wawili kabla hajafunguka ukurasa wa kuzaa. Mshindi huyo Tusker Project fame amesema kwa sasa yupo mbioni kumtafuta mwanaume wa ndoto yake ili waweze kufunga pingu ya maisha. Kutokana na changamoto ya kumtafuta mchumba Ruth matete amesema huenda akatumia njia za kitabibu kupata watoto mapacha na njia hiyo isipofanya kazi atamtafuta mwanaume ambaye yupo tayari kumsaidia kufanikisha ndoto yake hiyo. Utakumbuka Ruth Matete alijipata kwenye njia panda baada ya kumpoteza mume wake John Apewajoye kwenye ajali ya moto Hata hivyo baada mume wake kufariki watu walimshambulia mitandaoni wakidai huenda alihusika moja kwa moja kwenye kifo cha mume wake huyo madai ambayo aliyekana.

Read More