Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Juma Jux, ameachia rasmi kazi yake mpya ya muziki, EP iitwayo “A Day To Remember”, kama kumbukizi maalum ya ndoa yake na mkewe mpendwa, Priscy. Kupitia mitandao ya kijamii, Jux ameeleza kuwa mradi huu si kazi ya kawaida, bali ni simulizi ya maisha yao ya upendo, kuanzia mwanzo wa safari yao ya mahaba hadi furaha waliyonayo sasa kama wanandoa. EP hiyo imejaa hisia, utamaduni na usanii wa hali ya juu, ikiwa imeshirikisha mastaa wawili wakubwa: Phyno kutoka Nigeria na D Voice kutoka Tanzania. Jux ameamua kuunganisha ladha ya Afrika Mashariki na Magharibi ili kuwasilisha ujumbe wa upendo unaovuka mipaka ya lugha na mataifa. Kati ya watayarishaji walioweka mikono yao kwenye kazi hii ni S2kizzy, Foxx Made It, na Aykbeats, huku kazi ya mixing na mastering ikifanywa na Lizer Classic, jina kubwa katika ubora wa sauti Afrika. Katika ujumbe wake, Jux hakusita kumshukuru mkewe Priscy kwa kuwa chanzo cha msukumo wa EP hii, pamoja na familia yake, timu nzima ya wasanii na wahusika waliounga mkono kazi hiyo, na mashabiki waliomfuatilia kwa miaka mingi. Amesisitiza kuwa baada ya harusi yao rasmi, atatoa wimbo wa kipekee kama zawadi ya kufunga sura hii mpya ya maisha. EP “A Day To Remember” itapatikana kuanzia usiku wa leo kwenye majukwaa yote ya kidijitali ya kusikiliza muziki. Mashabiki tayari wameonyesha hamasa kubwa, wakisubiri kwa shauku kusikia mchanganyiko wa upendo na sanaa katika kazi hii ya kipekee.

Read More
 Prodyuza kutoka Tanzania S2kizzy ashirikishwa kwenye Album ya Black Eyed Peas “Elevation”

Prodyuza kutoka Tanzania S2kizzy ashirikishwa kwenye Album ya Black Eyed Peas “Elevation”

Mtayarishaji wa Tanzania S2kizzy ameshiriki kwenye kuitayarisha Album mpya ya Kundi maarufu la Muziki duniani Black Eyed Peas “Elevation” ambayo imetoka rasmi wiki hii. Zombie ameshiriki kutayarisha wimbo namba 9 kwenye Album hiyo uitwao “Filipina Queen” ambao ameshirikishwa mwanadada Bella Poarch. Kwenye Album hiyo yenye vyuma 15, Black Eyed Peas wamewapa mashavu wakali wa dunia kama Shakira, Ozuna, David Guetta, Daddy Yankee na wengine. Kundi hilo linaundwa na wasanii wanne akiwemo William James Adams Jr, Allan Pineda Lindo (apl.de.ap), Jaime Luis Gomez (Taboo) na J. Rey Soul. Kundi hilo lilifanikiwa kuitikisa dunia na Hit single yao “Where Is The Love” mwaka 2003.

Read More
 MAPRODYUZA WA BONGOFLEVA S2KIZZY NA BLACQ WATOFAUTIA KIMAWAZO KUHUSU SUALA LA MIRAHABA

MAPRODYUZA WA BONGOFLEVA S2KIZZY NA BLACQ WATOFAUTIA KIMAWAZO KUHUSU SUALA LA MIRAHABA

Watayarishaji wawili wa muziki kutoka nchini Tanzania Blacq Beatz na S2kizzy wameonekana kutofautiana katika mtazamo wa maprodyuza kutohusika katika mgao wa mirabaha ya muziki iliyotolewa usiku wa kuamkia Januari 29. Hili limekuja baada ya Chama cha Hakimiliki Tanzania COSOTA kwa kushirikiana na wizara ya sanaa kutoa sehemu ya fedha zilizopatikana kwenye kazi za wanamuziki {mirabaha} huku watayarishaji wa muziki wa Bongofleva wakisahaulika kwenye orodha hiyo. S2kizzy ameonekana kutofurahishwa na jambo hilo huku Blacq akijibu kuwa jambo hilo limetokana na wao kama maprodyuza kutojua thamani na haki yao, ambapo amesema maprodyuza wa Bongofleva waendelee kusubiri kusaidiwa na wasanii.

Read More