Rapa Khaligraph Jones Akanusha Madai ya Sabato Kuhusu Simu

Rapa Khaligraph Jones Akanusha Madai ya Sabato Kuhusu Simu

Rapa maarufu wa Kenya Khaligraph Jones amekanusha vikali madai yaliyotolewa na mchekeshaji na mtoaji maudhui mtandaoni Sabato, maarufu kama “Sauti ya Ground”, kuwa alikaidi ombi la msaada wa simu. Akizungumza kupitia mahojiano na SPM Buzz, Khaligraph alieleza kuwa hajawahi kupokea ombi hilo kutoka kwa Sabato, wala hajawahi kuonana naye ana kwa ana kwa lengo hilo.  “Anajua Sabato, buda buda, hujakuja ofisi yangu kuniambia nikununulie simu bro. Najua mambo zako bro, lakini hata kwa field yako, watu kama wewe wanahitajika kukamilisha mzunguko,” Alisema kwa msisitizo. Khaligraph aliongeza kuwa amekuwa akimnyamazia Sabato kwa muda mrefu, licha ya kusikia na kuona kauli mbalimbali mitandaoni. Hata hivyo, alisema amefikia hatua ya kuweka mambo wazi kwa sababu ya kuenea kwa maelezo yanayoweza kupotosha mashabiki. “Nilikuwa nimekunyamazia for the longest time. Najua mambo zako bro, lakini hakuna kitu Sabato. Hakuna mtu anaweza kusema kitu juu ya OG saa hii,” Aliongeza. Khaligraph aliweka wazi kuwa hajawahi kukataa kumsaidia mtu yeyote mwenye shida halisi, lakini hakubaliani na wale wanaotumia jina lake mitandaoni kwa kiki au kutafuta huruma ya mashabiki. Mpaka sasa, Sabato hajatoa tamko lolote rasmi kujibu kauli ya Khaligraph. Hata hivyo, mashabiki na wanamitandao wameanza kujadili suala hilo kwa makini, huku wengi wakisubiri iwapo Sabato atajibu au kuomba radhi.

Read More