MWALIMU RACHAEL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU KUITAPELI KUNDI LA SAILORS GANG

MWALIMU RACHAEL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU KUITAPELI KUNDI LA SAILORS GANG

Aliyekuwa meneja wa Sailors Gang Mwalimu Rachael amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya msanii Cocos Juma kumtuhumu kuwa alipora shillingi millioni 15 za kundi hilo. Kupitia chaneli yake ya Youtube Mwalimu Rachael amesema ameshangazwa na kitendo cha Cocos Juma kumzushia taarifa za uongo kuwa aliwatapeli pesa zao ikizingatiwa kipindi anasimamia muziki  wao alihakikisha kila msanii wa kundi hilo anafaidi na mirahaba ya nyimbo zao. Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba masaibu yanayowaandama wasanii wa Sailors Gang yametokana na wao kumpuuza alipowakataza kujiunga na lebo ya Black Markert Records ambayo imesambaratisha kimuziki. Mwalimu rachael amefichua kwamba wasanii hao wamekuwa wakijaribu kumuomba msamaha arudi afanye nao kazi lakini amekataa ombi lao kutokana na wao kumharibia brand yake kwa kumzushia taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo amedokeza mpango wa kuwatambulisha wasanii wake wapya chini lebo yake ya muziki ya MRX Media licha ya wasanii wa Sailors kumharibia jina na hata kumkatisha tamaa kwenye suala la kuwasimamia wasanii.

Read More
 KRG THE DON AFUFUA BIFU YAKE NA KUNDI LA SAILORS GANG

KRG THE DON AFUFUA BIFU YAKE NA KUNDI LA SAILORS GANG

Msanii wa  muziki nchini KRG The Don amefufua tena bifu yake na wasanii wa sailors gang siku chache baada msanii wa kundi hilo Cocos Juma kudai kuwa lebo ya Black Market Records imesambaratisha muziki wao. Kupitia ukurasa wake wa instagram KRG The Don amesema aliwaonya wasanii wa sailors gang kuhusu muziki wao lakini walimchukulia poa huku akienda mbali zaidi na kusema kwamba tamaa ya kutaka maisha ya haraka ndio imewaponza wasanii hao jambo ambalo analodai lilipelekea kuingia mkataba na lebo ya Black Market Records ambayo iliwapoteza kimuziki. Bosi huyo wa Cash group Entertainment amedai masaibu yanayowaandama wasanii wa Sailors ni kutokana na kiburi waliowaonyesha wadau wa muziki nchini kipindi walipata umaarufu kubwa kwenye tasnia ya muziki nchini. Hata hivyo amewataka wasanii wa Sailors Gang kuwaomba msamaha watu waliowadharau kipindi cha nyuma ili njia zao zianze kufunguka Ikumbukwe KRG The Don na Sailors Gang waliachia  wimbo  wa pamoja uitwao “Nyandus” mwaka wa 2019 lakini lilopokuja suala la kutayarisha video walizozana kuhusiana na ishu ya malipo  na hivyo  ikasambaratisha  mpango wa kuiachia video  rasmi ya wimbo huo.

Read More
 COCOS JUMA WA SAILORS GANG AFUNGUKA MANYANYASO WANAYOPITIA CHINI YA BLACK MARKET RECORDS

COCOS JUMA WA SAILORS GANG AFUNGUKA MANYANYASO WANAYOPITIA CHINI YA BLACK MARKET RECORDS

Msanii wa Sailors gang,Cocos Juma amedai kwamba wanajuta kujiunga na lebo ya muziki ya Black Market Records. Katika mahojiano na Plug TV Cocos Juma amekiri kutopata chochote kwenye muziki wao ikiwemo kutomiliki kazi zao za muziki ambazo wamezifanya kwa kipindi chote ambacho amekuwa chini ya lebo ya muziki ya black market records. Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba lebo hiyo inatumia wasanii kujipatia pesa huku ikiwaacha wakiishi maisha ya uchochole. Hata hivyo ametoa changamoto kwa serikali kuweka mikakati ya kuwalinda wasanii kutoka kwa matapeli kwani vijana wengi wamejipata wakitumia mihadarati baada ya kuporwa mamilioni ya pesa kupitia kazi zao za muziki. Ikumbukwe wasanii wa Sailors Gang waliingia mkataba na lebo ya muziki ya Black Market Records baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wao mwalimu Rachael na tangu wakati huo wamepotea kimuziki.

Read More
 MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Member wa kundi la Sailors gang, Shalkido ametangaza kuachana kabisa na masuala ya muziki. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram,Shalikido amesema amechukua uamuzi huo baada ya kugundua kuwa muziki wake umepoteza mvuto kwenye jamii, hivyo ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee. “Baada ya muda mrefu kutafakari kuhusu kazi yangu ya muziki, nimegundua kuwa muziki wangu hauna mashiko.” “Kwa hivyo nimeamua kubadilisha kazi yangu kwa kufanya kitu kitakachoniridhisha zaidi maishani. Kwa mashabiki wangu wote walioniamini, samahani sana kuwaangusha.”, Ameandika kupitia instastory yake. Taarifa Shalkido kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya kutaka kusilikiza nyimbo za kundi la Sailors gang. Baadhi ya mashabiki wa shalkido wanahisi huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini ili aweze kuachia singo yake mpya.

Read More
 SAILORS GANG WATANGAZA UJIO MPYA

SAILORS GANG WATANGAZA UJIO MPYA

Kundi la muziki wa Gengetone Sailors Gang limetangaza kurejea rasmi kwenye game ya muziki nchini baada ya ukimya wa miaka miwili. Wasanii wanaounda kundi hilo wamethibitisha taarifa hiyo kwenye mahojiano yao ya hivi karibuni huku wakiwataka mashabiki zao wakae mkao wa kula kupokea ujio wao mpya ambao wameutaja ni wa kitofauti sana ikizingatiwa kuwa wana mpango wa kuachia ngoma mfululizo bila kupoa. Wasanii hao wamekanusha tetesi za kuacha muziki kama inavyoripotiwa mitandaoni ila walichukua mapumziko mafupi kwa ajili ya kujipanga vizuri kimuziki. Ikumbukwe kundi la Sailors Gang ambalo linaundwa na wasaani Miracle Baby,Masilver na Shalkido lilijipatia umaarufu mwaka wa 2019 kupitia muziki wa gengetone ambao unapendwa na vijana wengi nchini.

Read More