MWALIMU RACHEL AISIMAMISHA TWITTER KWA TUHUMA ZA KUISAMBARATISHA KUNDI LA SAILORS GANG

MWALIMU RACHEL AISIMAMISHA TWITTER KWA TUHUMA ZA KUISAMBARATISHA KUNDI LA SAILORS GANG

Aliyekuwa meneja wa kundi la Sailors Gang Mwalimu Rachel ameusimamisha mtandao wa Twitter kwa Jina lake kukaa namba 9 kwenye orodha ya ‘Topics’ ambazo zinazungumzwa zaidi kwenye mtandao huo nchini Kenya. Hadi sasa mtandao huo unaonesha jina la  Mwalimu Rachel  limeongelewa kwenye zaidi ya Tweets 2,562 ikiwa ni masaa machache tu tangu member wa Sailor Gangs, Miracle Baby afunguke mazito kuhusu menejimenti yake ya zamani ambayo ilikuwa inasimamiwa na mwanahabari huyo. Akijibu swali la shabiki aliyeulizia kuhusu ukimya wa kundi la Sailors , Miracle Baby Miracle Baby alidai kuwa ukimya wao umetokana na hatua ya Mwalimu Rachel kuwafanyia figisu ya kuwashusha kimuziki ikiwemo kuwanyang’anya akaunti zao za mitandao ya kijamii na kuaharibi dili za mamilioni ya fedha ambazo walikuwa wapewa na makampuni mbali mbali. Hata hivyo jambo hilo limeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wameonekana kumtupia lawama mwalimu Rachel kwa hatua ya kuwafanyia figisu wasanii wa Sailors wasiendelee kimuziki huku wengine wakiwalaummu wasanii hao kwa kuingia mkataba na kampuni ya mwanahabari huyo bila kumshirikisha wakili. Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka wa 2020 Mwalimu Rachael na Sailors Gang waliingia kwenye mgogoro mara baada ya wasanii wa kundi hilo kijiunga na lebo ya muziki ya Black Market Records bila  ya kumhusisha meneja wao ambaye kwa wakati huo alikuwa Mwalimu Rachel. Mwanamama huyo alienda mbali zaidi na kuchukua akaunti za mitandao ya kijamii ya wasanii wa Sailors Gang hadi pale wasanii wa kundi hilo watakapomlipa shilllingi milllioni 1.5 kama fidia ya kusimamia kazi zao za muziki.

Read More