Harmonize amshukuru Sallam SK kumtaja namba 10 kwa wasanii waliofanya vizuri 2022

Harmonize amshukuru Sallam SK kumtaja namba 10 kwa wasanii waliofanya vizuri 2022

Hitmaker wa “Outside”, Msanii Harmonize ameshukuru meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK kwa kumuweka kwenye orodha ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022. Kupitia insta story yake amemshukuru Sallam SK kwa kumtaja namba 10 katika list yake ambapo ameenda mbali zaidi na kujifananisha na mchezaji nyota Duniani, Lionel Messi ambaye huvaa jezi namba kumi mgongoni. “Thank You Kipara no Mara Waa!!!!. 10. MESSI+”, Ameandika. Siku ya jana Sallam SK alitoa list yake ya wasanii 10 wa Bongo Fleva waliofanya vizuri mwaka 2022, akiwapanga kuanzia nafasi ya 1 mpaka ya 10.

Read More
 Babu Tale akanusha madai ya Sallam SK kujiunga na Lebo ya Konde Music Worldwide

Babu Tale akanusha madai ya Sallam SK kujiunga na Lebo ya Konde Music Worldwide

Meneja wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi kwa ujumla, Babu Tale amesema sio kweli kwamba Sallam SK anajiunga na Lebo ya Harmonize, Konde ‘Gang’ Music Worldwide. Tale amesema amefurahi kuona wawili hao wamemaliza tofauti zao kama ilivyoonekana mitandaoni hivi karibuni lakini sio kweli suala kujiunga na Lebo yake. “Lakini nilipoona juzi wanasalimiana maana yake hakuna shida, ila hii ya kusema Sallam SK kakumbatiana na Harmonize anaenda Konde Gang, eeh, we kuweza!” amesema Babu Tale akiongea na Mjini FM. Itakumbukwa, Sallam anahusishwa zaidi kuwa ndiye atakaye kuwa Meneja wa Harmonize kufuatia video inayowaonesha wawili hao wakisalimiana na kukumbatiana walipokuwa visiwani Zanzibar ambapo Sallam alihudhuria kwenye show ya Harmonize jambo ambalo limeibua hisia chanya kwa mashabiki. Sallam SK ni miongoni mwa Mameneja wa watatu wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi, wengine ni Babu Tale na Mkubwa Fella.

Read More
 Meneja wa Diamond, Sallam SK ajibu disstrack ya Harmonize

Meneja wa Diamond, Sallam SK ajibu disstrack ya Harmonize

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam SK amemjibu Harmonize kufuatia mashairi yake kwenye wimbo “Champion” alioshirikishwa na rapa Kontawa. Harmonize kwenye sehemu fupi ya wimbo huo aliimba kwamba, kwa sasa Konde Gang ni Jeshi la watu wawili akiwa na maana kwamba ni yeye na Ibraah pekee yaani baada Killy, Cheed na Anjella kujiondoa. Sallam ama Mendez leo Jumanne kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kwamba, “Kwa hiyo kaua lebo kafungua kundi, wanajiita.. “Wagambo mtu mbili” au nimeelewa vibaya ” ameandika kupitia ukurasa wake. Utakumbuka tangu ameondoka WCB Wasafi, Harmonize hajawa na wakati mzuri na Lebo hiyo hasa Sallam SK ambaye mara kadhaa wameonekana kupisha kauli mtandaoni na hata walipokutana.

Read More
 JOH MAKINI AMTOLEA UVIVU SALLAM SK KISA NGOMA YA DON’T BOTHER ALIYOMSHIRIKISHA RAPA AKA

JOH MAKINI AMTOLEA UVIVU SALLAM SK KISA NGOMA YA DON’T BOTHER ALIYOMSHIRIKISHA RAPA AKA

Msanii wa Hip Hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amekanusha vikali madai ya Sallam SK kuhusu kolabo yake na Rapa wa Afrika Kusini, AKA. Katika show ya The Joint ya Dizzim TV, Sallam SK alidai kuwa yeye ndiye aliyeunganisha kolabo ya Joh Makini na AKA (Don’t Bother) bila malipo yoyote. Joh Makini kupitia mtandao wa Twitter ameonyeshwa kushangazwa na kauli hiyo, huku akimtaja mtu anayetambulika kama ‘Mwarabu’ kufanya mpango wa kukwamisha kolabo hiyo. “Aeleze aliunganisha vipi, kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki wa Pili na G Nako lakini waliomleta walikuwa hawataki itokee” amesema. “Yeye sio chanzo cha hiyo collabo. Mwarabu alipambana sana kukwamisha hii basi tu Mwenyenzi Mungu huwa hajawahi kushindwa,” amesema Joh Makini. Utakumbuka ngoma ya Don’t Bother ambayo Joh Makini kamshirikisha AKA ilitoka Novemba mwaka wa 2015 chini ya Producer, Nahreel, video yake ilifanyika Afrika Kusini, Director wake ni Justin Compas kutoka Gorilla Films.

Read More