Sam West awataka watu kutoingilia mahusiano yake na Vivian
Siku moja baada ya Sam West kuthibitisha kuwa mahusiano yake na mwimbaji Vivian yameingiwa na ukungu, sasa mchekeshaji huyo ambaye anasusua kisanaa nchini ameibuka na mpya. Kupitia mitandao ya kijamii Sam West amewataka watu kutoingilia sana sakata la ndoa yake na Vivian kuvunjika kwani huenda wakabaki njia panda ikitokea wamefufua tena penzi lao. “Methali: Mambo ya watu wawili waliopendana usiyaingilie, utaachwa katikati wakirudiana.” Ameandika Instagram. Ujumbe huo umetafsiriwa na walimwengu kuwa huenda ni kiki ya ujio mpya wa Vivian kimuziki ambapo amewataka wawili hao kuachia wimbo huo mara moja badala ya kudanganya umma kuwa jini mkata kamba ameingilia mahusiano yao. Sam West na mke wake Vivian wamekuwa gumzo mtandaoni baada ya taarifa kuibuka kuwa wawili hao wamebwaga manyanga. Utakumbuka Vivian ndiye alikuwa wa kwanza kuweka wazi kuwa anapitia wakati mgumu akitaka mashabiki wamweke kwa maombi baada ya mume wake kumkimbia licha ya kujaribu kutatua tofauti zao. Haikushia hapo Sam West pia alitumia mitandao yake kijamii kudokeza kuwa ndoa yake imefikia mwisho kwa kile alichokitaja kutoelewana kati yake na mke wake Vivian.
Read More