Msanii Maarufu wa Mugithi Samidoh Aaga Rasmi Huduma ya Polisi

Msanii Maarufu wa Mugithi Samidoh Aaga Rasmi Huduma ya Polisi

Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS) imekubali rasmi kujiuzulu kwa mwanamuziki maarufu wa Mugithi, Samuel Muchoki, anayejulikana kwa jina la kisanii Samidoh. Samidoh, ambaye amehudumu katika jeshi la polisi kwa miaka 12, alitoa barua ya kujiuzulu akitaja sababu binafsi na hamu ya kuzingatia kikamilifu taaluma yake ya muziki inayozidi kung’aa. Kujiuzulu kwake kumeanza kutekelezwa kuanzia Julai 20, na hatua hiyo imempa uhuru wa kuendelea na kazi yake ya muziki bila vikwazo vya majukumu ya kikazi. Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Edward Mbugua Kanja alisema Samidoh sasa yuko huru kufuata kile anachokitaka na kwamba huduma ya polisi inamtakia kila la heri katika maisha yake mapya. Samidoh alijiunga na polisi mwaka 2013 na kwa miaka yote hiyo alifanikiwa kusawazisha majukumu ya kazi na safari yake ya muziki. Umaarufu wake katika uimbaji wa Mugithi ulimfanya kuwa kati ya wasanii wachache walioweza kutamba kwenye sanaa huku bado akiwa mtumishi wa serikali. Kujiuzulu kwake sasa kunampa nafasi ya kuwekeza nguvu na muda wote katika muziki, ambapo tayari amejijengea mashabiki lukuki ndani na nje ya Kenya. Wachambuzi wa tasnia ya muziki wanasema hatua hii huenda ikafungua ukurasa mpya katika safari ya Samidoh, wakitarajia kutoa nyimbo zaidi, kufanya maonesho makubwa na hata kupanua upeo wa kimataifa.

Read More
 Samidoh Aingia Matatani Baada ya Kushiriki Nderemo za ‘Wantam’ Klabuni

Samidoh Aingia Matatani Baada ya Kushiriki Nderemo za ‘Wantam’ Klabuni

Mwanamuziki na afisa wa polisi, Konstebo Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, anaripotiwa kuwa katika hatari ya kupoteza ajira yake baada ya kushiriki nderemo na vifijo vya “Wantam” akiwa kwenye klabu ya burudani. Kwa mujibu wa Huduma ya Polisi Nchini (NPS), Samidoh anadaiwa kukiuka mwongozo rasmi unaodhibiti mwenendo wa maafisa wa polisi, hata wanapokuwa nje ya majukumu ya moja kwa moja. NPS imethibitisha kuwa suala hilo linachunguzwa, na endapo Samidoh atapatikana na hatia, anaweza kuadhibiwa kwa njia mbalimbali, zikiwemo kupokonywa wadhifa, kuhamishwa kituo, kutozwa faini, kupewa onyo la kinidhamu au hata kuachishwa kazi kabisa. Tukio hilo limezua maoni mseto mitandaoni, huku mashabiki wake wakimiminika mitandaoni kumuunga mkono kwa kusema ana haki ya kuwa na maisha ya kibinafsi nje ya kazi. Wengine hata wameeleza kuwa Samidoh ni kiungo muhimu katika kuunganisha jamii kupitia muziki wake wa Mugithi na haoni sababu ya kuadhibiwa kwa kuonyesha furaha na burudani. Hata hivyo, NPS imesisitiza kuwa maafisa wa polisi wanawajibika kudumisha nidhamu na taswira ya heshima, hata wanapokuwa nje ya kazi, na kwamba utii wa kanuni za huduma ni wa lazima kwa wote. Samidoh, ambaye amejizolea umaarufu kwa kuunganisha taaluma ya uaskari na muziki, bado hajazungumzia rasmi tukio hilo. Huku uchunguzi ukiendelea, mashabiki wake wanasubiri kwa hamu kuona iwapo atapewa onyo, kuhamishwa, au hatimaye kuachishwa kazi.

Read More
 Akaunti ya youtube ya msanii Samidoh yarejeshwa baada ya kudukuliwa

Akaunti ya youtube ya msanii Samidoh yarejeshwa baada ya kudukuliwa

Akaunti ya Youtube ya mwanamuziki wa mugithi Samidoh imerejeshwa hewani baada ya kufutwa kwa kukiuka sheria za mtandao huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Samidoh ameshindwa kuficha furaha yake kwa kuchapisha ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake na pia kuwataka mashabiki zake waendelee kumuonyesha upendo kupitia kazi zake za muziki. Kaunti ya youtube ya Samidoh  ilifunguliwa rasmi Mei 11 mwaka 2011 na mpaka sasa ina jumla ya watazamaji millioni 47. Samidoh kwa sasa yupo nchini Marekani kwa ziara ya kimuziki iliyoanza Oktoba 2022 ambapo inatarajiwa kukamilika Disemba 3 mwaka huu.

Read More