Uhamisho wa Samidoh Wazua Taharuki, Ujumbe Wake Waacha Maswali

Uhamisho wa Samidoh Wazua Taharuki, Ujumbe Wake Waacha Maswali

Msanii mashuhuri wa Mugithi na afisa wa polisi, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha ujumbe tata kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, muda mfupi baada ya kuhamishwa kazini. Kupitia Instagram, Samidoh aliandika: “When injustice becomes law, resistance becomes duty!”, kauli yenye uzito inayohusishwa na upinzani dhidi ya udhalimu. Ujumbe huo umetafsiriwa na wengi kama ishara ya kutoridhishwa na hatua ya uhamisho wake kutoka Makao Makuu ya Polisi wa Mkoa wa Kati hadi Kitengo Maalum cha Kukabiliana na Wizi wa Mifugo (ASTU) kilichopo Gilgil, Kaunti ya Nakuru. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, uhamisho wa Samidoh unahusishwa na tukio la Mei 16 ambapo alionekana akitumbuiza huku umati ukipiga kelele za kisiasa ya “Wantam”,  kauli inayodaiwa kupinga utawala wa Rais Ruto. Tukio hilo lilisambaa sana mitandaoni. Ingawa Inspekta Jenerali Douglas Kanja alieleza kuwa uhamisho huo ni wa kawaida, taarifa za ndani zinaeleza kuwa ni hatua ya kinidhamu kwa kukiuka kanuni zinazokataza polisi kushiriki katika siasa. Mashabiki wa Samidoh wamegawanyika baadhi wakimtia moyo kuendelea na kazi ya polisi kwa nidhamu, huku wengine wakimtaka aachane na kazi hiyo na kujikita kikamilifu katika muziki, ambapo tayari ameonyesha mafanikio makubwa. Kwa sasa, Samidoh anasubiri matokeo ya uchunguzi wa kinidhamu, hatua inayoweza kuathiri mustakabali wake katika Jeshi la Polisi. Ujumbe wake wa mafumbo unaendelea kuibua mjadala mpana, huku wengi wakisubiri kwa hamu kuona hatua atakayochukua kama msanii, raia, au afisa wa sheria.

Read More
 Karen Nyamu afunguka baada ya kuzua tafrani nchini Dubai

Karen Nyamu afunguka baada ya kuzua tafrani nchini Dubai

Baby Mama wa mwanamuziki wa Mugithi Samidoh Muchoki, Karen Nyamu amezungumzia kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akiwa anasindikizwa na walinzi nje ya ukumbi wa tamasha la Samidoh huko Qatar. Akizungumza moja kwa moja kwenye mtandao wa Instagram, Karen Nyamu amesema hakuwa na habari kuwa alihitaji leseni ya kuonekana jukwaani. Katika utetezi wake, amesema hakufanya kosa lolote kwenda jukwaani kwani alikuwa akifurahia tu burudani kama mashabiki wengine. Seneta huyo mteule ameongeza kuwa chini ya shinikizo ya kilevi, hivyo maazimio yake ya 2023 ni kuacha kunywa pombe kabisa. “Pombe inanifanya nisahau njia, Nimeacha Pombe.” Kwenye instagram live, shabiki mmoja alimshauri aache kufuata Samidoh ambapo alijibu kwamba anahitaji maombi ili kukomesha mzaha maishani mwake. Karen Nyamu pia aliwataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi naye. “Niko na Kila kitu kitu sina ni haya.” Akijibu moja ya shabiki yake, aliongeza kuwa hana mpango wa kuachana na Samidoh kwa sababu ya malezi ya watoto wao wawili kwa pamoja. “Simuachi, lazima Tulee watoto.”

Read More
 Karen Nyamu azua purukushani kwenye tamasha la Samidoh Dubai

Karen Nyamu azua purukushani kwenye tamasha la Samidoh Dubai

Seneta mteule  Karen Nyamu amejipata katika hali ya aibu baada ya kujaribu kujiunga na baba wa mtoto wake Samidoh Muchoki jukwaani alipokuwa akitumbuiza nchini Dubai. Kwenye video inayosambaa sana katika mitandao ya kijamii, Karen Nyamu ameonekana akivamia jukwaa ambalo Samidoh alikuwa akitoa burudani kwa mashabiki katika jaribio la kujiunga na mwanamuziki huyo wa Mugithi. Samidoh hata hivyo hakumpa muda wa kuzua purukushani ambapo walinzi wake walimsindikiza Karen Nyamu nje. Katika video hiyo, Samidoh alisimama akiwatazama maafisa wa usalama wakimsindikiza mama ya mtoto wake nje. Kisha akamkumbatia mkewe Edday Nderitu kwa upendo huku wakipiga picha na mashabiki. Siku chache zilizopita, Samidoh na mkewe walisafiri nchini Dubai kwa ajili ya hafla ya sherehe ambapo alitarajiwa kutumbuiza pamoja na wanamuziki wengine. Mama ya mtoto wake Karen Nyamu pia alijikatia tiketi ya ndege kujiunga nao kwenye sherehe hiyo ya mwisho wa juma. Mashabiki wengi walikasirishwa na hatua ya Karen kuhujumu safari ya Samidoh-Edday kwa kusema kwamba alimkosea heshima mke mkuu wa mwanamuziki huyo.

Read More