Sammy Boy Akanusha Taarifa za Gari Lake Aina ya Mercedes Benz GLE 53 Kupigwa Mnada

Sammy Boy Akanusha Taarifa za Gari Lake Aina ya Mercedes Benz GLE 53 Kupigwa Mnada

Msanii na Mjasiriamali kutoka nchini Kenya, Sammy Boy, amezungumza wazi kuhusu uvumi ulioenea kwamba gari lake la kifahari aina ya Mercedes Benz GLE 53 lilipigwa mnada kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Katika video aliyoshiriki kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sammy Boy amekanusha vikali madai hayo, akieleza kuwa gari hilo halikupigwa mnada bali alilirejesha kwa muuzaji mwenyewe baada ya kugundua kuwa lilikuwa na matatizo ya gearbox (gia) yaliyokuwa yakijirudia mara kwa mara. “Nilinunua gari hilo kwa uaminifu mkubwa, lakini baada ya muda mfupi nilianza kupata changamoto kwenye mfumo wa gia. Baada ya mashauriano na muuzaji, niliamua kulirudisha kwa hiari ili kuepuka matatizo zaidi,” alieleza Sammy Boy. Sammy By ambaye pia ni Mshawishi maarufu wa mitandao ya kijamii, amesisitiza kuwa hatua hiyo haikuwa kwa sababu ya matatizo ya kifedha kama inavyodaiwa mitandaoni, bali ni uamuzi wa kibiashara na wa kiusalama. Aliongeza kuwa bado anaendelea na shughuli zake za biashara kama kawaida na hana deni lolote linalohusiana na gari hilo. Mashabiki wake wengi wameonyesha kumuelewa na kumpongeza kwa uwazi wake, huku wengine wakihimiza umuhimu wa wanasoshalaiti kuwa wa kweli na kufafanua mambo yanapovuma mtandaoni. Hata hivyo kampuni iliyomuuza gari hilo haijatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo hadi sasa.

Read More
 Sammy Boy Afichua Kujitambua Upya Kisanii, Aahidi Kuwachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

Sammy Boy Afichua Kujitambua Upya Kisanii, Aahidi Kuwachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Sammyz Boy, ametoa kauli ya kuvutia kupitia mtandao wa Instagram, akieleza jinsi alivyogundua upya kipaji chake katika kuandika na kuimba muziki. Kupitia InstaStory, Sammy Boy alisema kuwa baada ya kusikiliza kazi zake mwenyewe, alitambua kiwango chake cha ubunifu na uwezo aliokuwa ameupuuza kwa muda. Katika ujumbe huo, Sammy Boy aliandika:  “I listened to my music and I realized how talented I am in both writing and singing. I felt motivated and I noticed I have been silent on my doing. I will drop a banger soon enough.” Kauli hiyo imechukuliwa kama dalili ya kurejea kwake rasmi kwenye tasnia ya muziki, ambapo mashabiki wake wameonyesha msisimko na matarajio makubwa kupitia maoni na ujumbe wa kuhamasisha kwenye mitandao ya kijamii. Sammy Boy, ambaye awali alijulikana kwa mitindo ya kipekee na uandishi wa mashairi yenye hisia halisi, amekuwa kimya kwa muda katika ulingo wa muziki. Hata hivyo, ujumbe wake wa hivi karibuni unaashiria kuwa msanii huyo anajiandaa kurudi na wimbo mpya, ambao ameuahidi kuwa ni “banger”. Wadadisi wa tasnia ya muziki wanasema kuwa hali ya msanii kujitathmini binafsi ni hatua muhimu ya ubunifu na ukuaji wa kisanaa, na hatua ya Sammy Boy inaweza kuwa mwanzo wa awamu mpya katika taaluma yake. Mashabiki wake sasa wanasubiri kwa hamu tangazo rasmi la tarehe ya kuachia wimbo huo mpya.  

Read More