Samsung Yatoa Uhuru Mpya kwa Watumiaji Kupitia Quick Settings

Samsung Yatoa Uhuru Mpya kwa Watumiaji Kupitia Quick Settings

Kampuni ya teknolojia ya Samsung imeanza kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa uendeshaji, ikilenga kutoa uhuru zaidi kwa watumiaji kupitia toleo jipya la One UI 8.5. Mabadiliko haya makuu yanahusu sehemu ya Quick Settings na Lock Screen, ambazo sasa zitakuwa completely customizable, hatua inayoashiria ushindani wa moja kwa moja na mfumo wa iOS wa Apple pamoja na ule wa Google Pixel. Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Samsung, watumiaji wataweza kupangilia kila sehemu ya Quick Settings, kuchagua ukubwa wa vitufe, kuweka mpangilio wa sections wanavyotaka, na hata kubadilisha namna muonekano wa Lock Screen unavyoonekana. Hii ni mara ya kwanza kwa Samsung kuruhusu kiwango hiki cha uhuru katika muundo wa mfumo wake, hatua inayoonesha dhamira ya kampuni hiyo kuimarisha uzoefu wa mtumiaji. Maboresho haya yanaifanya One UI 8.5 kuwa ya kipekee zaidi, huku ikitoa nafasi kwa watumiaji kuunda muonekano wa simu zao kwa mtindo wa kipekee kulingana na ladha na mahitaji yao. Samsung inalenga kuvutia zaidi wapenzi wa ubinafsishaji (customization) ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na uwezo wa Pixel n iPhone katika maeneo hayo. Kwa sasa, mabadiliko haya yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika simu mpya zitakazokuja na One UI 8.5, kabla ya kusambazwa kwa masasisho kwenye baadhi ya vifaa vya zamani vya Samsung.

Read More
 Samsung Kubadilisha Mtindo wa Watermark Katika Picha za Kamera

Samsung Kubadilisha Mtindo wa Watermark Katika Picha za Kamera

Samsung imepanga kuleta mabadiliko makubwa katika namna watermark (alama ya utambulisho) huonekana kwenye picha zinazopigwa kwa simu zake. Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya style ya watermark tangu kutolewa kwa toleo la One UI 5.0. Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja, mfumo mpya wa One UI 8.5 unakuja na style mpya ya watermark ambayo ni ya kina zaidi na ya kipekee ikilinganishwa na ile ya sasa. Tofauti na watermark ya awali ambayo ilikuwa rahisi na yenye maelezo machache, watermark mpya itaonyesha taarifa nyingi zaidi kuhusu picha husika. Katika style hii mpya, watermark itaonekana upande wa kushoto chini ya picha, huku upande wa kulia ukiwa na maelezo ya kiufundi kama aina ya lensi, ISO, focal length, exposure value, aperture, shutter speed, pamoja na tarehe na muda halisi ambao picha imepigwa.  Mabadiliko haya yanachukuliwa kama jitihada za Samsung kuboresha utambulisho wa picha na kuwapa wapiga picha taarifa zaidi kwa ajili ya kumbukumbu au matumizi ya kitaalamu. Hata hivyo, baadhi ya watumiaji mtandaoni wameanza kutoa maoni wakidai kuwa style hii mpya inafanana sana na ile ya makampuni kama Vivo na Xiaomi, ambayo tayari yanaweka watermark zenye maelezo ya kina kama hayo katika picha zao. Licha ya ukosoaji huo, mashabiki wa Samsung wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mfumo mpya wa One UI 8.5 utakavyoboresha uzoefu wa matumizi ya kamera kwenye simu hizo, hasa kwa wapiga picha wanaopenda maelezo ya kiufundi moja kwa moja kwenye picha zao.

Read More
 Samsung Yaanza Kutoa Toleo Jipya la Mfumo wa One UI 7 kwa Galaxy A53

Samsung Yaanza Kutoa Toleo Jipya la Mfumo wa One UI 7 kwa Galaxy A53

Kampuni ya Samsung imeanza kutoa toleo jipya la mfumo wa One UI 7 kwa watumiaji wa simu ya Galaxy A53. Mfumo huu mpya umejengwa kwa kutumia Android 15 na una ukubwa wa takriban GB 3.4. Baadhi ya watumiaji duniani tayari wameanza kupokea marekebisho haya ya mfumo, na watumiaji wa Afrika Mashariki wanatarajiwa kuupata katika siku chache zijazo. Ili kuepuka matatizo wakati wa upakuaji, watumiaji wanashauriwa kuhakikisha kuwa wana nafasi ya kutosha kwenye simu na kutumia Wi-Fi yenye kasi nzuri. Toleo hili jipya linaleta maboresho mbalimbali kama vile muonekano mpya wa simu, ulinzi wa juu wa usalama, na mabadiliko kwenye skrini ya kufungua simu (lock screen), yote yakiwa na lengo la kuboresha matumizi ya kila siku ya simu.

Read More