Samuel Eto’o aomba radhi kwa kumshambulia Mwandishi wa Habari

Samuel Eto’o aomba radhi kwa kumshambulia Mwandishi wa Habari

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o ameomba radhi kufuatia kitendo chake cha kumpiga na kumshambulia kwa mateke Mwandishi wa Habari mnamo Disemba 5 mwaka huu. Kwenye video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya Kijamii, Eto’o alionekana akimshambulia Mwandishi huyo ambaye ni raia wa Algeria. “Ningependa kuomba radhi kwa kushindwa kuzuia hasira zangu na kufanya kitendo ambacho hakiendani na utashi wangu.” ameandika Eto’o. Kwenye msamaha huo ambao ameutoa hadharani, Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cameroon alitueleza kisa cha kwanini alifikia uamuzi huo wa hasira na kumpiga Kijana huyo. Amesema ni chuki na maneno ya dhihaka ambayo yanaendelea toka kwa mashabiki na Wananchi wa Algeria kufuatia kuondolewa na Cameroon kwenye kuwania tiketi ya ushiriki wa Kombe la Dunia 2022. Tangu ushindi wa mabao (2-1) na Cameroon kupita kwa sheria ya bao la Ugenini March 29 mwaka Jana, vita, uhasama na chuki vimekuwa vikimuandama Samuel Eto’o toka kwa mashabiki wa Algeria wakidai kwamba Cameroon ali-cheat pasina ushahidi wowote. Aidha ameliomba Shirikisho la Soka nchini Algeria pamoja na mamlaka husika kukomesha hili kabla ya majanga makubwa hayajatokea.

Read More
 Samuel Eto’o amshushia kichapo cha mbwa mpiga picha Qatar

Samuel Eto’o amshushia kichapo cha mbwa mpiga picha Qatar

Rais wa chama cha soka nchini Cameroon na mchezaji wa zamani wa Timu ya Inter Milan, Barcelona n.k Samuel Eto’o amshushia kichapo Mpiga picha Mjongeo (Videographer) baada ya kutoka kutazama mchezo wa Kombe la Dunia kati ya Brazil na Korea Kusini. Baada ya kutoka Uwanjani Eto’o alionekana kupiga picha na mashabiki nje ya Uwanja wa 974 nchini Qatar na baadae alitokea Mtu aliyeshika kamera ambapo alionekama kuzungumza jambo na Eto’o. Dakika Chache baadae Eto’o alionekana kushikwa na hasira na kuanza kumshambulisha jamaa huyo. Pamoja na kuzuiwa na watu Eto’o alifanikiwa kumpiga na kufanikiwa kumdondosha chini jamaa huyo. Mpaka sasa haijafahamika ni sababu gani iliyopelelea Eto’o kumshushia kichapo jamaa huyo.

Read More