Sanaipei Tande Kuaga Sanaa Baada ya Miaka Zaidi ya Ishirini Katika Tasnia

Sanaipei Tande Kuaga Sanaa Baada ya Miaka Zaidi ya Ishirini Katika Tasnia

Msanii mkongwe na mwenye kipaji cha kipekee, Sanaipei Tande, amefichua kuwa yuko katika hatua za kutafakari kuachana na sanaa na muziki ili kufuatilia masuala mengine maishani mwake. Katika mahojiano ya hivi karibuni, Sanaipei alieleza kuwa ingawa sanaa na muziki vimempa jina na mafanikio, amefika mahali ambapo anahisi ni wakati wa kufanya mambo mengine. “Nafikiria kuacha muziki na sanaa ili nijaribu vitu vingine maishani. Kuna maisha zaidi ya jukwaa na kamera,” alisema Sanaipei kwa utulivu lakini kwa uhakika. Mashabiki wengi wameonyesha masikitiko yao mitandaoni, huku wengine wakiheshimu maamuzi yake na kumtakia mafanikio katika safari yake mpya. Hadi sasa, Sanaipei hajafichua ni nini hasa anapanga kufanya baada ya kuachana na muziki, lakini amesisitiza kuwa ni uamuzi alioufikiria kwa kina na unaoendana na malengo yake ya kibinafsi. Sanaipei alianza safari yake ya muziki miaka ya 2000 na amejizolea sifa kwa sauti yake ya kipekee na uwezo wa kuandika mashairi yenye hisia. Mbali na muziki, amewahi pia kung’ara kwenye vipindi vya redio, uigizaji wa tamthilia, na filamu. Iwapo ataachana rasmi na sanaa, bila shaka atakumbukwa kama mmoja wa wasanii wa kipekee waliotoa mchango mkubwa katika muziki wa Kenya. Mashabiki wake sasa wanasubiri kwa hamu kujua hatua yake inayofuata.

Read More
 PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

Rapper Prezzo, Sanaipei tande na Mchekeshaji maarufu nchini ambaye pia ni mgombea wa ubunge langat  Jalang’o wametajwa kuwa miongoni mwa mastaa 10 na wachekeshaji 17 wa kenya  ambao watarajiwa kushirikishwa  kwenye show mpya ya ucheshi iitwayo Roast House. Show hiyo inalenga kusherekea mafanikio na machango wa mastaa mbali mbali nchini Kenya kupitia ucheshi ambao utafanywa na kundi la wachekeshaji wa majukwaani. Roast House ina maonyesho au Episodes 10 za dakika 24 kila moja ambayo itawapa nafasi kwa wachekeshaji kutoa burudani na vichekesho wakiangazia madai, kauli mbiu na matukio mbali mbali maishani kwa ajili mastaa watakao kuwa wamealikwa. Roast House ambayo itaruka hewani Julai 14 mwaka huu imetayarishwa na eugene mbugua kwa ushirikiano na D & R studios pamoja na makundi ya wachekeshaji kutoka nchini Kenya.

Read More
 SANAIPEI TANDE ATEULIWA KUWANIA TUZO YA WOMEN IN FILM AWARDS 2022

SANAIPEI TANDE ATEULIWA KUWANIA TUZO YA WOMEN IN FILM AWARDS 2022

Staa wa muziki nchini Sanaipei Tande ameteuliwa kushiriki  kwenye tuzo za Women in Film Awards (WIFA) kwa mwaka wa 2021. Sanaipei ametajwa kuwania kipengele cha TV Drama akichuana na waigizaji kama Ann Stella Karimi, Jacky Matubia,Mercy Mueni, Ann Stella Karimi na Michelle Chebet Tiren. Tayari zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua washindi wa vipengele mbali mbali linaendelea hadi Februari 15 mwaka wa 2022 kupitia mitandao ya kijamii ya Women In Film Awards. Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya nne nchini Kenya zilianzishwa kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika tasnia ya  filamu ambayo inazidi kukua kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Read More
 SANAIPEI TANDE AWAANIKA MAPROMOTA NA MADEEJAY WA KENYA WANAOMTAKA KIMAPENZI KABLA YA KUMPA SHOWS

SANAIPEI TANDE AWAANIKA MAPROMOTA NA MADEEJAY WA KENYA WANAOMTAKA KIMAPENZI KABLA YA KUMPA SHOWS

Msanii kike nchini Sanaipei Tande amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kudai kuwa mapromota na madeejay wa Kenya wamekuwa wakimtaka kimapenzi kabla ya kumpa nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemtaka sanaipei tande aweke wazi majina ya mapromota na madeejay hao wanaoendeleza kadhia hiyo ili wasanii wachanga waweze kuwaepuka. Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Sanaipe Tande alikiri hadharani kuwa kuna mmoja wa wanahabari tajika nchini alimtaka kimapenzi ili ampe michongo itakayobadilisha maisha yake.    

Read More