Mzozo Mpya Wazuka Kati ya Weasel na Mkewe Sandra Teta

Mzozo Mpya Wazuka Kati ya Weasel na Mkewe Sandra Teta

Mwanamuziki wa Uganda, Weasel Manizo, na mkewe Sandra Teta wamejikuta tena katika mzozo mkali, miezi miwili tu baada ya tukio la awali ambapo inadaiwa Teta alimgonga kwa gari. Tukio jipya limeibuka kupitia video iliyosambaa usiku wa kuamkia jana, ikimuonyesha Weasel akiwa katika hali ya taharuki huku akilia akiomba msaada. Katika video hiyo, Teta anaonekana akijaribu kumshambulia Weasel kwa kifaa kikali, wakati ndugu wa familia wakijitahidi kumzuia. Ingawa Teta alisikika akikanusha kumdhuru mumewe, bado haijabainika chanzo cha mzozo huo mpya. Weasel, akionekana mwenye hofu kubwa, alimshutumu mkewe kwa kumtesa na kumtaka aondoke nyumbani kwake, akisema hana tena amani naye. Hali hii imewafanya mashabiki na wadau wa muziki kuhoji mustakabali wa ndoa yao, hasa ikizingatiwa kuwa si mara ya kwanza wawili hawa kuingia katika ugomvi wa hadharani. Mnamo Julai mwaka huu, Teta alidaiwa kumgonga Weasel kwa gari katika baa moja eneo la Munyonyo, tukio lililosababisha msanii huyo kulazwa katika Hospitali ya Nsambya akiwa na mguu uliovunjika. Teta alikamatwa na polisi, lakini aliachiwa baada ya Weasel kuamua kutofungua mashtaka dhidi yake.

Read More
 WEASEL MANIZO AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUMPIGA MKE WAKE

WEASEL MANIZO AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUMPIGA MKE WAKE

Mwanamuziki Weasel Manizo amefunguka kwa mara ya kwanza baada taarifa za kumshushia kipigo cha mbwa mke wake Sandra Teta kusambaa mtandaoni. Akizungumzia tukio hilo, Weasel amekanusha vikali tuhuma za kumpiga mke wake kwa kusema kwamba hahitaji msaada wa mtu yeyote katika kuitunza familia yake. Haikushia hapo ameenda mbali na kusema kwamba ni jambo la kushangaza kuona watu wanamkosoa mtandaoni ilhali wana migogoro katika familia zao. “Karibu kila familia ina matatizo, mbona unanizungumzia mimi kana kwamba unanijali kuliko mimi? Ninaishi maisha bora na mke wangu na sihitaji msaada wa mtu yeyote katika masuala kama haya. Geuza nguvu zako kwenye mambo mengine,” ameelezea akiwa kwenye moja ya shoo yake usiku wa kuamkia leo. Duru za kumianika zinadai kuwa wazazi wa Sandra Teta walisafiri kutoka Rwanda hadi Uganda kwa ajili ya kumuokoa binti yao kutokana na manyanyaso aliyokuwa anapitia kwenye ndoa yake.

Read More
 SANDRA AMTAKA DANIELLA ATIM KUTOINGILIA NDOA YAKE NA WEASEL

SANDRA AMTAKA DANIELLA ATIM KUTOINGILIA NDOA YAKE NA WEASEL

Baby mama wa msanii Weasel, Sandra Teta amemtaka mke wa Jose Chameleone’, Daniella Atim akome kuingilia masuala ya mahusiano yake. Daniella Atim amekuwa akiendesha kampeini ya kutaka haki itendeke kwa sandra teta ambaye aliripotiwa kushushiwa kipigo cha mbwa na mume wake Weasel manizo. Lakini Sandra ameonekana kutopendezwa na kitendo cha Daniella kumtetea kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba aache kufuatilia maisha yake ya ndoa na badala ashughulike na familia yake. Hata hivyo Daniella Atim kupitia ukurasa wake wa Instagram amemjibu Sandra kwa kusema kwamba aache kujifanya ilhali anaumia moyoni kutokana na kichapo alichopewa na baby daddy wake Weasel Manizo. Daniella ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anaelewa sandra bado anapitia kipindi kigumu katika maisha yake, hivyo anapaswa kusaidiwa kimawazo ili arejee katika hali yake ya kawaida.

Read More