Sarah Mtalii Afafanua Kuhusu Video Yake na Simon Kabu: “Hatujarudiana, Tulikuwa Kazi Tu”

Sarah Mtalii Afafanua Kuhusu Video Yake na Simon Kabu: “Hatujarudiana, Tulikuwa Kazi Tu”

Mfanyabiashara maarufu Sarah Mtalii ametoa ufafanuzi kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimuonesha akiwa na aliyekuwa mumewe, Simon Kabu, akisema wazi kuwa haikuwa safari ya kimapenzi bali ya kibiashara. Kupitia taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari, Sarah alieleza kuwa video hiyo imechukuliwa visivyo na umma, huku wengi wakidhania kuwa wawili hao wameamua kurejeana kimapenzi. Hata hivyo, Sarah amesisitiza kuwa wao bado hawajarudiana na kwamba mchakato wa talaka yao bado unaendelea mahakamani. “Ilikuwa ni safari ya kibiashara, si kitu kingine. Sisi si wapenzi tena, na talaka yetu inatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Julai,” alisema Sarah kwa uwazi. Taarifa hiyo imekuja baada ya mashabiki wengi kueleza mshangao wao kuona wawili hao wakiwa pamoja, huku baadhi wakipeleka tetesi kuwa huenda wametatua tofauti zao. Hata hivyo, Sarah amesema licha ya kutengana kimapenzi, wanaendelea kushirikiana kibiashara kwa sababu ya maslahi ya pamoja na familia. Simon Kabu bado hajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo au kauli ya Sarah, lakini wadadisi wa mitandao wanazidi kufuatilia kwa karibu hatua za wawili hao.

Read More