Taylor Swift Aandika Historia kwa Kurejesha Haki za Muziki Wake

Taylor Swift Aandika Historia kwa Kurejesha Haki za Muziki Wake

Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Taylor Swift, ametangaza rasmi kwamba amepata tena umiliki rasmi kazi zake za awali, hatua kubwa inayohitimisha miaka ya mapambano kuhusu haki ya umiliki wa kazi za wasanii. Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, Taylor alieleza furaha yake baada ya kurejesha umiliki wa albamu zake sita za mwanzo, ambazo awali zilikuwa chini ya lebo ya Big Machine. Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Swift aliwashukuru kwa uungwaji mkono waliompa katika kipindi chote cha changamoto. “Sasa ninamiliki muziki wangu. Asante kwa kusimama nami, safari hii haingekuwa na maana bila ninyi,” aliandika. Ameeleza kuwa hatua hii si tu ya kihistoria binafsi, bali ni mfano kwa wasanii wengine kuhusu umuhimu wa kumiliki kazi zao. “Hili ni jambo kubwa sana kwangu na kwa kila msanii anayepigania haki zake,” aliandika Taylor Taylor Swift sasa anamiliki kikamilifu albamu zake maarufu kama Fearless, Speak Now, Red, 1989, Taylor Swift (debut), na Reputation ambazo zilimjengea jina kubwa kimataifa. Wengi wa mashabiki wake wamesherehekea ushindi huu kama hatua ya haki na mafanikio dhidi ya mfumo wa muziki unaowanyima wasanii udhibiti wa kazi zao. Mnamo mwaka 2019, lebo ya muziki ya Big Machine iliuza katalogi yake ya muziki kwa meneja wa muziki Scooter Braun, ambaye baadaye aliuzia kampuni ya uwekezaji ya Shamrock Capital  bila ridhaa wala ushiriki wa Swift. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa kimataifa kuhusu haki za wasanii katika tasnia ya muziki, huku Taylor akichukua hatua ya kurekodi upya albamu zake ili kupata tena udhibiti wa kisheria.

Read More
 Justin Bieber Bado Anadaiwa Mamilioni na Meneja Wake wa Zamani Scooter Braun

Justin Bieber Bado Anadaiwa Mamilioni na Meneja Wake wa Zamani Scooter Braun

Nyota wa muziki wa pop Justin Bieber bado anadaiwa mamilioni ya dola na meneja wake wa zamani Scooter Braun, licha ya wawili hao kusitisha rasmi uhusiano wao wa kikazi takribani miaka miwili iliyopita, vyanzo vya karibu na suala hilo vimedokeza. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia vyanzo vya karibu na wasanii hao wawili, deni hilo linahusiana na makubaliano ya kifedha yaliyokuwa ndani ya mkataba wa usimamizi kati ya Bieber na Braun, ikiwa ni pamoja na mgao wa mapato kutoka miradi ya awali ya muziki, matangazo ya biashara, na makubaliano ya udhamini yaliyosainiwa kabla ya kutengana kwao. Scooter Braun aligundua kipaji cha Justin Bieber mwaka 2007 kupitia video ya YouTube na kisha kumsainisha kwenye lebo ya Raymond Braun Media Group (RBMG), ikishirikiana na Island Records. Kwa zaidi ya muongo mmoja, Braun alisimamia safari ya Bieber kutoka kuwa kijana mdogo hadi kuwa miongoni mwa wasanii wanaouza zaidi duniani. Mnamo mwaka 2023, ilithibitishwa kuwa Bieber na Braun hawakuwa tena wakifanya kazi pamoja. Taarifa hiyo iliwashangaza wengi kwenye tasnia ya muziki, hasa ikizingatiwa ukaribu wao wa muda mrefu. Hata hivyo, hakuna upande uliotoa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuvunjika kwa mkataba huo. Chanzo kimoja kilichoomba kutotajwa jina kililiambia shirika moja la habari la burudani kuwa, “Kuna masuala ya kifedha ambayo hayajakamilika tangu walipoachana. Scooter anaamini ana haki ya kulipwa fedha alizopaswa kupata kutokana na kazi aliyofanya kwa miaka mingi.” Ingawa hakuna uthibitisho kuwa suala hilo limefikishwa mahakamani, vyanzo vinasema kuna uwezekano wa kufunguliwa kwa kesi iwapo pande husika hazitafikia makubaliano ya maridhiano. Wachambuzi wa sheria za burudani wanasema kuwa ni jambo la kawaida kwa madeni ya aina hii kuibuka hasa pale ambapo mikataba ilikuwa na vipengele vya malipo ya baadaye (deferred earnings). Mmoja wa wataalamu wa sheria za muziki jijini Los Angeles alisema:  “Mikataba ya usimamizi wa wasanii huwa na vipengele vinavyoruhusu meneja kuendelea kulipwa hata baada ya mkataba kuvunjika, mradi mapato hayo ni matokeo ya kazi iliyofanywa wakati wa usimamizi wao.” Hadi kufikia sasa, Justin Bieber hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu madai haya. Msanii huyo amekuwa akionekana mara chache hadharani na hivi karibuni alionekana kuendelea na maisha ya faragha pamoja na mkewe Hailey Bieber. Katika miezi ya hivi karibuni, Bieber amekuwa akiashiria kurejea kwenye muziki kupitia mitandao ya kijamii, lakini hakutoa tarehe rasmi ya kurejea studio au kutoa albamu mpya.

Read More