Senegal Kuchuana na Congo Kundi D CHAN

Senegal Kuchuana na Congo Kundi D CHAN

Mabingwa watetezi wa mashindano ya soka ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani, Senegal, wataangazia kuandikisha ushindi wao wa pili mtawalia katika mechi dhidi ya Congo, itakayochezwa leo katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mchuano huo wa Kundi D umepangwa kuanza saa 5:00 jioni. Senegal iliifunga Nigeria 1-0 katika mechi yao ya ufunguzi na sasa inalenga kuongeza pointi dhidi ya Congo, ambayo katika mechi yake ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1 na Sudan. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Senegal na Congo kukutana katika mashindano ya CHAN, ingawa timu hizo zimefuzu mara nne katika historia ya mashindano haya. Mchezo mwingine wa kundi hili utaunganisha Nigeria dhidi ya Sudan, na utakamilika kuanzia saa 8:00 usiku. Kwa sasa, Senegal inaongoza Kundi D kwa alama tatu, ikifuatiwa na Sudan na Congo zenye alama moja kila moja, huku Nigeria ikiwa nyuma baada ya kupoteza mechi yake ya ufunguzi.

Read More
 Senegal yaondolewa Kombe la Dunia

Senegal yaondolewa Kombe la Dunia

Wawakilishi wa Afrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia timu ya Taifa ya Senegal imeondoshwa kwenye hatua ya 16 bora ya mashindano hayo baada ya kupokea kichapo kizito cha 3-0 kutoka kwa England Jordan Henderson na Harry Kane waliifungia England katika kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa na Bukayo Saka mwanzoni mwa kipindi cha pili. Kocha wa Senegal Aliou Cisse anasema walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia hasa baada ya katikati ya kipindi cha kwanza, Krépin Diatta aliingilia pasi mbaya kutoka kwa Harry Maguire na krosi yake ikasababisha hati hati kwenye lango la Uingereza. Ismaila Sarr alipiga krosi ya ikagongwa mwamba wa Jordan Pickford na kutoka nje. Wakati huo huo Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia timu ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya robo ya fainali baada ya kuizaba Poland 3-1 katika mchezo wa 16 Bora Kylian Mbape alifunga mara mbili na kutoa pasi moja ya mwisho kwa Olivier Giroud aliyeweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa muda wote kwenye kikosi cha Ufaransa kwa kufikisha mabao 52 Ufaransa sasa atakutana na  England  kwenye hatua ya robo fainali

Read More
 England kukutana na Senegal kwenye hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2022

England kukutana na Senegal kwenye hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2022

Timu ya Taifa ya Senegal imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Ecuador katika mchezo wa mwisho wa kundi A Matokeo hayo yameifanya Senegal kumaliza wa pili katika kundi hilo kwa kufikisha alama 6 nyuma ya Uholanzi waliomaliza wakiwa vinara na alama 7 baada ya kuwazaba wenyeji Qatar 2-0 katika mchezo mwingine wa kundi hilo. Wakati huo huo Timu ya Taifa ya England imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Dunia kwa kuizaba Wales 3-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B Mabao mawili ya Marcus Rashford na moja la Phil Foden yametosha kuipa alama zote tatu England na kumaliza vinara kwenye msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 7 Sasa England atakutana na wawakilishi wa Afrika timu ya Taifa ya Senegal kwenye hatua ya 16 bora

Read More
 Wenyeji Qatar waondolewe kwenye michuano ya Kombe la Dunia

Wenyeji Qatar waondolewe kwenye michuano ya Kombe la Dunia

Wenyeji wa michuano ya Kombe la timu ya Taifa ya Qatar imekuwa timu ya kwanza kuondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Senegal kwenye mchezo wa pili wa kundi A. Simba wa Teranga Senegal imewatoa kimasomaso Waafrika kwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika kupata ushindi kwenye michuano hiyo ya mwaka huu na kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano kutoka katika kundi hilo. Qatar watakamilisha ratiba tu katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo kwa kuwavaa Uholanzi.

Read More