Promota Abtex afunguka kutomsamehe Serena Bata
Promota wa muziki kutoka nchini Uganda Abtex amefunguka kuwa hana mpango wa kumsamehe msanii serena bata licha ya msanii huyo kusimama naye kipindi anatoka gerezani. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema bado ana machungu na serena kwa kuvunja mkataba wa kufanya naye kazi licha ya kuwekeza mamilioni ya pesa kusimamia muziki wake. “Niliwekeza zaidi ya milioni 300 kwa Serena. Nilikuwa na ndoto kubwa lakini alisambaratisha kila kitu nilipopata changamoto kadhaa. Alikimbia kwa mwanasheria na kuomba kuvunja mkataba wetu. Alianza kunifanyia mambo machafu.”, Alisema. Abtex amedai kuwa hivi karibuni atamchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo ili aweze kulipa fedha zote alizotumia kugharamia muziki wake. “Kwa kweli, huwezi kucheza na pesa zangu hivyo. Ningekuwa nimejenga nyumba kwa pesa yangu lakini niliwekeza kwake. Nina maumivu makali na namchukia sana. Nitachukua hatua kali za kisheria hivi karibuni,” Abitex alielezea Utakumbukwa Promota Abtex alitoka jela kwa dhamana mapema wiki hii na Serena Bata alikuwa moja kati ya watu waliojitokeza kumpokea na kumuonyesha upendo. Wawili hao walifanya kazi pamoja lakini walivunja mkataba wao mwaka jana na wakaanza kuwa maadui. Kwa Serena, kwenda kusimama na Abitex wakati wa matatizo ilikuwa ni ishara kuweka kando tofauti zao, lakini kwa Abitex bado ana machungu na mrembo huyo.
Read More