B Classic akiri kutamani penzi la mwanasholaiti maarufu mtandaoni Shakilla
Msanii B Classic ameweka wazi matamanio ya kumchumbia mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya Shakilla kwa kigezo kuwa lazima awe mlokole. Kupitia instastoy yake amesema yuko tayari kuingia kwenye mahusiano na Shakilla huku akidai kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa mrembo huyo anafurahia maisha yake ya ndoa. “Shakila ! I have seen unataka kutoka soko – Niko soko pia and I can take you in. Na nikupe maisha poa Tu. Ila are you willing to change? I’ll cater for everything. Bora tu nione unakua church girl. Haijalishi it will take how long,” Aliandika Instastory. Kauli ya B Classic imekuja mara baada ya Shakilla kukiri hadharani kuwa hakuna shabiki yake anayetaka kuingia naye kwenye mahusiano ambayo yataishia kuwa ndoa. βSo outta all of my followers, no one wants to enter into a serious relationship with me. Was I meant to be in the streets for life?β aliandika Instastory. Ikumbukwe mwezi mmoja uliopita Shakilla alidai kuwa hatokuja kuchumbiana na wanaume wa Kenya ambapo alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa heri atoke kimapenzi na wanaume wa Nigeria kutokana na ukarimu wao.
Read More