Shakira aweka rekodi kwenye mtandao wa Youtube
Mwimbaji nyota duniani Shakira ameuanza mwaka 2023 kwa kuvunja rekodi ya muda wote ya mtandao wa Youtube hii ni kufuatia wimbo wake mpya uitwao “BZRP MUSIC SESSION 53” kuwa wimbo wa Ki-Latin uliotazamwa kwa muda mfupi zaidi katika mtandao huo tangu video itoke. Inaelezwa kuwa, video ya wimbo huo ilipata views Milioni 63 kwa saa 24 na pia ikapata views Milioni 125 ndani ya siku 4 pekee. Hiyo inatajwa kuwa ni rekodi ya aina yake. Wimbo huo ni Disstrack kwa Baba watoto wake Gerald Pique ambaye ni mchezaji mstaafu wa klabu ya Barcelona, wamebarikiwa watoto wawili nao ni Milan (9) na Shasha (7), na waliachana mwaka jana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka 10.
Read More